Utangoja sana mpaka kukutana na mtandao kama huoKipindi cha nyuma kidogo Halotel walikua na bando ya gb10 kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi na mbili alfajiri. Na sio Halotel tu, hata mitandao mingine ilikua na bando za usiku pia ambazo zilikua spesho sana kwa kushushia mizigo mikubwa kama movies na files nyingine zenye size kubwa. Kwa sasa ni kama hamna mtandao wenye bando ya usiku.
Kwa wazee wa kushusha movies, mnatumia bando ipi na ya mtandao gani kwa sasa kushushia movies?
Natumia Voda, kuhusu kula bando kihalali hata Voda wanakula kihalali. Natumia App ya Internet Meter inanionyesha matumizi ya mb ambayo simu yangu inatumia. Hesabu za mb zinaenda sawa kabisa na za mtandao. Ishu saivi ni mitandao ya kijamii ambayo watu wanatumia sana inakula sana mb, Instagram, Tik Tok n.kKwa sasa mkombozi wangu ni TTCL.... Hawana ofa ya maana ila tofauti yake ni kwamba data zao zinalika kihalali.... Mfano nikiwa na GB 3 naweza kushusha muvi ya GB2.5 ikamalizika bila shida yoyote na zikabakia angalau MB300, hizo MB200 zinaweza potea kama slippage...
Mitandao mingine mfano Voda nikiwa na GB3 naweza download GB1.5 tuu kisha bando linakata... Ukijiuliza hizi GB1.5 zingine zimepotelea wapi huwezi kuelewa...
TTCL wana ofa yao moja ya BUFEE ambapo kwa 15K unapata 10GB..... Ndiyo nayoiona ni nafuu kwangu kwa sasa.