Msaada: Ni namna gani naweza pata taarifa zangu za NIDA zilizotumika wakati wa usaili?

SlimFit

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2016
Posts
2,041
Reaction score
3,119
Wakuu amani iwe nanyi.

Twende kwenye mada, ni namna gani naweza pata taarifa zote za namba yangu ya NIDA bila kufika NIDA?

Kwanini bila kufika NIDA?

Nimeona kabisa jamaa ananijaza i.e anasema taarifa zangu za education hazipo kwa mfumo hivyo natakiwa nimtafute nijaze fomu nifanye maombi upya. Kwangu mimi bado haiingii akilini niliona nisibishane nae ili nisipoteze muda wangu. Mwisho akaniandikia taarifa chache tu.
 
Kwamba namba ya nida unayo ama kitambulisho unacho lakini zile taarifa zako hakuna? Ajabu kidogo.

Swali la msingi mlikuwa katika mazingira gani ama ilikuwaje kuwaje mpaka akudai taarifa zako za msingi?
 
Tulikua ofisini kwao, Kitambulisho nilikua nacho alichokifanya akaingiza namba kupata details, hapo ndio shida ikaanza. Akasema taarifa kama namba ya simu, education, etc hazipo kwa mfumo kwahiyo natakiwa kujaza upya.

Ukumbuke hapo nimekwama kuna process naifanya Brela sasa inahitaji makercheker kwenye NIDA, na NIDA kupitia jamaa ndio wanaleta hizo stori.
 
Unga tela, wenzako wanasubiri majibu

1721488390105.png

1721488431914.png
 
Tulikua ofisini kwao, Kitambulisho nilikua nacho alichokifanya akaingiza namba kupata details, hapo ndio shida ikaanza. Akasema taarifa kama namba ya simu, education, etc hazipo kwa mfumo kwahiyo natakiwa kujaza upya.

Ukumbuke hapo nimekwama kuna process naifanya Brela sasa inahitaji makercheker kwenye NIDA, na NIDA kupitia jamaa ndio wanaleta hizo stori.
Namba zilizopo ktk kitambulisho chako waweza hakika kama ndizo kwa njia mbalimbali
-Brela
-TRA
-Mitandao ya Simu
Nk

Ni wewe kuchngamsha akili
 
Mkuu nachohitaji mimi ni taarifa zangu zilizojazwa kwenye mfumo i.e elimu, anuani za makazi, nilipojiandikishia n.k

Kwa kutumia hizo njia ulizo ainisha hapo juu, nitapata vipi hizo taarifa?
 
Nilikuwa naomba usaidizi kama naweza kuangalia taalifa zangu za usajili nizojiandikishia kwenye NIDA kupitia namba yangu ya NIDA mtandaoni, muongozo huo tafadhali..
 
Wakuu amani iwe nanyi.

Twende kwenye mada, ni namna gani naweza pata taarifa zote za namba yangu ya NIDA bila kufika NIDA?

Kwanini bila kufika NIDA?

Nimeona kabisa jamaa ananijaza i.e anasema taarifa zangu za education hazipo kwa mfumo hivyo natakiwa nimtafute nijaze fomu nifanye maombi upya. Kwangu mimi bado haiingii akilini niliona nisibishane nae ili nisipoteze muda wangu. Mwisho akaniandikia taarifa chache tu.
Unazipeleka wapi hizo taarifa nyeti Mkuu?, maana taasisi za serikali zinasomana hivyo huwezi kuchukua taarifa nje ya zilizopo kwenye mfumo.

Ingekuwa hazipo angekuambia urudi NIDA kurekebisha/kujaza hizo taarifa na sio kuzitoa kiholela ivyo. Labda kama anataka kuzitumia kiuhalifu hapo baadae. Chukua tahadhari Mkuu.

Nimeona umeongelea BRELA hapo, hata wao hawapokei taarifa za mfukoni bali wanazivuta kutoka NIN moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom