Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu kwa madawa dr. Batmanghelidj.
Kosa kubwa ambalo binadamu tumelifanya dhidi ya miili yetu mpaka sasa, ni kusubiri mdomo ukauke au kiu ndipo tunywe maji. Ni kama vile kusubiri katikati ya mchana jua likiwa limewaka, ndipo unamwagilia maji bustani au kutembea umbali mrefu na gari na kusubiri mpaka maji yaishe kabisa ndipo uongeze maji kwenye injini papo hapo!.
Madhara makubwa ya kiafya yatokanayo na upungufu wa maji (dehydration) ambayo siyo lazima yaoneshe kukauka kwa mdomo au kiu, yanajitokeza kabla ya mdomo au kiu kutokea.
Kimsingi kiu na mdomo kukauka, ni ishara za mwisho kabisa za mwili kupungukiwa maji, na ikiwa mtu anategemea ishara hizi ili kunywa maji, basi mtu huyo atakuwa anajikaribishia mauti yasiyo ya lazima, kwani anaulazimisha mwili kusambaziwa maji kwa mgawo kutokana na amri zinazotolewa na ubongo ili kusambazia maji mifumo mhimu zaidi ukiwemo ubongo wenyewe.
kwa siku huwa unakunywa maji kiasi gani?, je ni chunvi ipi unatumia, ile ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) au ile ya dukani ya unga?, maji ni suluhisho kwa kila ugonjwa, jisomee mwenyewe katika: http://maajabuyamaji2.artisteer.net/jitibu-kwa-kutumia-maji/