Msaada nichukue ipi kati ya Spacio new model au premio old model?

Etugro

New Member
Joined
Feb 14, 2022
Posts
4
Reaction score
6
Wakuu habari zenu?
Wakuu nimejichanga changa namimi natamani nivute chombo kimoja kati tajwa hapo juu.
Naomba maoni yenu kwa kuzingatia
1. Uimara
2. Upatikanaji wa vipuri
3. Ulaji wa mafuta
4. Iliyotulia barabarani
Sijawahi kuzitumia zote zaid ya kuziona kwa watu ila kutokana na mahitaji yangu nimeona zinanifaa kwa kua sina familia kubwa na sina safari za mikoani mara kwa mara.

Naomba kuwasilisha. Asante
 
Zote ni chaguo sahihi, maana zote ni corolla na zote ni gari zinazodumu kwa muda mrefu

Zaidi sana , zote vipuri vinapatikana kwa urahisi na bei poa.

So, ni suala tu la wewe kufanya uamuzi wa ipi ni chaguo lako

In terms of muonekano , interiors etc.

Lakini vyote vya muhimu na msingi, ni almost the same.


EAPGS
MAFIATI AREA
MBEYA TANZANIA
WHATSAPP ONLY
+255 682 274 097
 
Asante sana mkuu kwa maoni yako
 
Kama ni Me, chukua Premio, hutojuta! I hope 2007 model is old model--- I recommend!
 
Mkuu chukua premio ni imara kuliko spacio japo mambo mengine yanafanana
 
Mimi ningekushauri uchukue Spacio new model kwa sababu zifuatazo:
1. Ni gari ina space ya kutosha ndani.
2. Nyingi zina 7seats
3. Stylish design yake inavutia zaidi kwa miundo ya magari madogo ya kisasa (Hivyo utakuwa unakwenda na wakati, kujisikia ukiwa barabarani, kujivunia kuwa unamiliki gari na pia hutasumbuka sana ukitaka kuiuza)
4. Comfortable and luxurious.
 
1. Uimara (Premio old model)✔
2. Upatikaji wa vipuri (Zote sawa)
3. Ulaji wa mafuta kidogo (Spacio new model)✔
4. Iliyotulia barabarani (Spacio new model)✔
 
Kwa ushauri wangu go for spancio new model ,old model kwa sasa hapana aisee

sent from HUAWEI
 
Kwani Premio haziuziki??
 
kama ni mutu ya family, na mbeba mazagazaka kupeleka home, chukua spacial, pili sio gari ambayo mvua ikinyesha mpaka utoke nje na mwavuli ndio u hukue kitu kwenye buti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…