Msaada: Nifahamisheni kimo sahihi cha paa la nyumba

Msaada: Nifahamisheni kimo sahihi cha paa la nyumba

Mbute na chai

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
564
Reaction score
593
Habari wakuu,

Kwa nyumba yenye ukubwa wa 13m kwa 12m (urefu na upana), ili iwe na mwonekano mzuri, urefu wa paa (king post height) unatakiwa uweje kwa kipimo cha futi?
 
Habari wakuu,

Kwa nyumba yenye ukubwa wa 13m kwa 12m (urefu na upana), ili iwe na mwonekano mzuri, urefu wa paa (king post height) unatakiwa uweje kwa kipimo cha futi?
Kutokana na span kuwa kubwa, ukitumia angle ya 45 paa litaenda juu sana ambapo kingpost height itabidi iwe 6m

Hapo nakushauri utumie angle ya 30 ambapo ili kupata height ya kingpost itabidi uchukue urefu wa wall plate (ambayo ni 12m) ugawanye na 3.5
Kingpost height = (12m/3.5) = 3.4m

Au ukiona angle 30 ipo chini kidogo, unaweza ukaongeza ikawa angle 35 ambapo factor ya kugawanyia itakuwa ni 3 so Kingpost height itakuwa ni 12m/3 ambayo ni sawa na mita 4

Kama unahitaji ramani, makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
 
Mafundi wa siku hizi wanaitafutia huko juu kwa juu. Yaani anasimamisha ubao anaanza kumuuliza mwenzake aliyechini 'hapo vipi'!

Akisema hapo poa, wanaanza kugongelea mbao. Hakuna tena habari za calculation
Nimecheka
 
Back
Top Bottom