Msaada: Nikipokea simu ya biashara mbele ya rafiki, ndugu au mke piga ua haifanikiwi, nifanyeje?

Msaada: Nikipokea simu ya biashara mbele ya rafiki, ndugu au mke piga ua haifanikiwi, nifanyeje?

Mcheza Viduku

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2020
Posts
1,111
Reaction score
2,754
Mimi ninafanya shughuli za kujiajiri mwenyewe, kitu ninachoshangaa ni pale nikiwa na rafiki/marafiki, ndugu au wife halafu nikapigiwa simu na mteja wangu tukaanza kupatana bei.

Baada ya hapo piga ua garagaza hiyo kamwe haitafanyika hata iweje, jambo hili limekuwa linaniumiza kichwa muda mrefu sana japo sijawahi kumwambia yyte kati yao kuwa wakisikiliza mazungumzo na wateja wangu basi biashara huwa inajamba.

Pia soma: Somo kwa Wanandoa - inawahusu waliooa na walioolewa tu

Wife yeye amekuwa mtu wa kulalamikia sana hili, maana ili kuepuka kuwa napoteza biashara nimebuni mbinu kwamba nikipigiwa simu ya kibiashara huku niko nae nasogea pembeni ili nikamalize mazungumzo.

Wajuvi wa mambo mnisaidie hili linaweza kuwa ni tatizo gani kwa watu wangu wa karibu
 
unalogwa kijana hio ilishawahi mtokea mdg wang tukampeleka kweny matibabu home kumbe kuna ndg ye2 alikua anafanya mambo. Ila saiv fresh ata akikaa na wife wake mambo yananyooka tu
 
Back
Top Bottom