Nimepata suluhisho 100%,
ilinilazmu ku google, moja ya sbb ikawa ni pengne mahnd yamekauka sanaa,
Kwenye punje ya mhind kwa ndani kwenye kile kimelea kunakua na unyevu unyevu hata km yamekauka,
ila km ile punje imetobolewa au kukauka kupitiliza basi ule unyevu unyevu hupotea wote,
mahind hupasuka sbb jinsi unavyo heat punje basi unyevu unyevu kdg uliopo ndani hugeuka kua mvuke, mvuke huu hutengeneza mkandamizo(pressure) kubwa ndan ya punje,
presure ikizid uwezo wa lile tabaka la juu(hull/pericarp) basi litapasuka na starch na proteins vinatoka.
kwaio punje ikfka juzi joto 180 C, pressure inapanda mpk 930 kPa, hapa lazma ipasuke.
Kwaio mahnd yangu mimi yalikua yamekauka kupitiliza, na nilinunua mifuko miwili kwaio ilinitoka 160k, nikawaza kuyatupa ni hasana,
nikajarb physics moja na ndio iliyoleta matokeo mazuri nikajua kumbe shida ni mahnd.
Nikachukua kikontena nikachota kdg nikayalaza kwenye fridge ya absorb ule ubaridi, asubuh nikatest,
matokeo yake yalipasuka ndani ya dk 2-3 bila kuungua,
Nikagundua pia kuungua kulikua kunasabishwa na kutopasuka.