tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,854
- 1,129
Kwanza nawasalimu wote!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, tatizo langu lilianza mwaka 2009/2010! Nakumbuka niliumwa, nikaenda dispensary nikaambiwa nina Malaria, nilipewa dawa..nilitumia lakini sikuona nafuu! Baada ya mwezi nilienda kupima nikaambiwa nina malaria tena, nikapewa dawa na ikawa hivyo karibia kila mwezi!
Nilitumia dawa nyingi sana, pia nilijitahidi kutumia chandarua ila bado nikawa muhanga wa malaria ya mara kwa mara! Mwaka 2010 mwishoni nilikuwa na daktari akashauri nilazwe niwekewe drips za quinin..nililazwa kwa siku tatu..nikaruhusiwa ila hali haikubadilika, hata nilipoenda kupima tena niliambiwa nina malaria..hali hiyo ilienda mpaka 2011/2012 ambapo nilikuja humu kuomba suluhu la tatizo langu, nilikuta topics nyingi sana za Malaria...kuna mdau alishauri ninunue dawa ya kihindi inaitwa Zandu, kiukweli Zandu ilinisaidia na Malaria ikawa mwisho wake!!
Mwisho wa malaria ukawa mwanzo tatizo jingine, typhoid na minyoo vikaanza kunisumbua..nimetumia dawa nyingi..nikawa napona ila sirudi katika ile hali ya mwanzo! Kuna wadau humu walinishauri nikafanye vipimo hospital kubwa, 2013 nilienda Regency...walichukua vipimo kadri walivyoona inafaa, mwisho wa siku daktari akadai sina tatizo lolote, nilimwambia lakini mimi naumwa..akanambia haiwezekani uumwe zaidi ya miaka miwili na uendelee kuishi, ungekuwa ushakufa!
Maisha yaliendelea huku mwilo ukiwa dhoofu, kazi za watu ikawa ngumu kufanya hali iliyopelekea kuacha kazi na kuamua kujiajiri!! Bado huku kwenye shughuri zangu nashindwa kuzifanya kwa ufanisi, pesa nyingi nazitumia katika kujitibu..maana haijawahi pita mwezi nikawa nipo salama kabisa!!
Mwaka huu nimefanya checkup ya HIV, January, April na May na matokeo yakawa negative! Ila bado hali ya mwili ni ile ile!
Hivi majuzi nimepima, nikaambiwa nina bacteria kwenye njia ya mkojo..nimepewa dozi ya Azuma..nimemaliza dozi ila hakuna nafuu yoyote, hapa tupo linasumbua..na muda wote najisikia kulala tu!
Wadau nateseka na hii hali, sijawahi lazwa hospital toka 2010, wala sijawahi umwa kiasi kwamba nikahitaji usaidizi wa mtu mwingine! Najitahidi kufata kanuni zote za usafi, ila hali ndo hiyo!
Najua humu kuna madaktari, na watu waliopitia hali kama yangu..naombeni msaada wenu ili nami niweze angalau kufurahia haya maisha!!
Natanguliza shukrani!!