Msaada: NIlianza kuumwa malaria, ikaja Typhoid, na sasa ni bacteria kwenye njia ya mkojo


Nenda kanisani ukaombewe yupo rafiki angu alifukuzwa kazi kwa sababu ya kuumwa kila wakati Mara malaria, typhoid alihangaika sana kama ww kumbe mapepo kaombewa kapona amepata kazi nzuri meneja Wa benk
 
Mimi nimewai kuugua tumbo nikapima nikaambiwa amiba..nikasumbuka na amiba weeee lakini ikawa ngumu kupona..yaani kila dawa nilitumia..lakini wapi.. tumbo liliendelea kuuma tu..kuna siku nilipima nikaambiwa sina ugonjwa..dokta akanambia dawa pekee ya ugonjwa wako ni KUNYWA MAJI MENGI.. NA MIMI NAKUPA USHAURI WA KUNYWA MAJI MENGI KILA SIKU..ata kama huyapendi kunywa kama dawa mwisho utazoea
 
Pole sana Mungu atakupinya, kaachini tafakari kama kuna mtu ulishamdhulumu, mwibia, mchukulia mke, mdhalilisha, demu uliemtakia kumuia ukamtosa n. k kuna watu vichwa vyao sio vyetu kwa jambo dogo hachelewi kukutenda. Ujikumbuka ukamuimbe msamaha. Tafuta yalipo maombi bila kujali dini yako ukaombewe na uwe na imani utapona. Pole sana.
 

asante kwa ushauri mkuu
 

Kwanza mkuu fahamu kwamba kuna aina fulani za magonjwa mwilini hayaponi kwa siku 1 au 2,inategemea mambo mengi sana.

Pili,usidharau kitu,hebu kuwa na mpangilio mzuri wa kula,kula vyakula kama dona,mboga za majani,matunda kwa wingi,maji ya kutosha.Epuka kunywa soda,pombe,juisi za viwandani,processed foods nk.Kula vya asili tu,nadhani unaelewa.

Kuna mdau mmoja amekushauri unywe juisi limao,basi fanya hivyo kila siku.Sina haja ya kuelezea limao lina faida gani kwa kirefu,lakini huweka damu kuwa kati hali ya usafi.

Kuwa na nidhamu ya kufanya hayo mambo kwa angalau mwezi mmoja au miwili.Ukiona hakuna mabadiliko rudi nitakuelekeza supplements za kutumia ili kuharakisha process ya uponaji.

Kutokana na maelezo yako nina uhakika itakuwa ni sumu tu mwili inayokusumbua.Ukiona huna nguvu ya kufanya mazoezi ujue kiwango cha kawaida cha voltage kwenye seli zako kimepungua,nguvu ni voltage katika seli.Sasa voltage imepungua kwa sababu ya hali ya acid iliyopo mwilini.Ushauri wa hapo juu umejikita kuondoa hali hiyo.

Pia kuhusu hizo machine za kuondoa sumu;inategemea umefanya mara ngapi kwa muda gani,ubora wa machine,upya wa machine,technician wa machine.Na baada ya kutoka kwenye machine ulikuwa unakula vyakula vya aina gani,yote haya ni muhimu ili kufanikisha ufanisi wa hiyo machine.

Mkuu tunahitaji kujua mengi sana,vinginevyo unaweza kusema umerogwa au una mapepo.Pole sana.

note:Kuna dawa za kuondoa sumu kwa haraka.Kama utafanikiwa kupata mtaalam mzuri basi unaweza kumaliza tatizo hilo kwa hara zaidi.Vyakula kama tangawizi,karoti,apples,stafeli,parachichi,bizari,kitunguu saumu,mafuta ya habbatus sauda,tango,juisi ya ubuyu,juisi ya mboga mbichi za majani kama spinachi na celery vinaweza pia kukuondolea sumu kwa haraka.

Suluhisho la tatizo lako liko hapo juu.
 
Hivi majuzi nimepima, nikaambiwa nina bacteria kwenye njia ya mkojo..nimepewa dozi ya Azuma..nimemaliza dozi ila hakuna nafuu yoyote, hapa tupo linasumbua..na muda wote najisikia kulala tu!

Hiyo Azuma itakuwa vizuri kama utakunywa kwa siku sita.
 
Mkuu tindikalikali, vipi hali yako? Tupe mrejesho mkuu. Ulipewa ushauri mwingi humu, je unaendeleaje
 
Last edited by a moderator:
minyoo na typhoid mmmh!! vipi huwa unapata proper dosage? na huwa unamaliza? maji ya kunywa unachemsha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…