Msaada: Nilitumia dawa za Malaria nikatokwa na malengelenge mwilini

sabri18

New Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
2
Reaction score
0
Wiki iliopita nilikua nasumbuliwa na mafua nikaenda kupima malaria nikawa nayo basi nikajiongeza nikaenda pharmacy nikanunua dawa metakeflin sijui ndo inaandikwa hivo haya

Baada ya kumeza usiku asubuhi naamka mwili wote unawasha macho yamekua mekundu siku inayofuata ndo hali ya kuungua kwenye ngozi na malenge lenge ikajitokeza nikaenda hosptal tena dokta kuniona na jinsi nilivomsimulia akanambia hyo ni allergy reaction iliotokea kwenye mwili hivo nna allergy na hizo dawa nikachomwa sindano ya kuondoa sumu ya dawa na dawa za kumeza nikapewa kwa ajili ya allergy hyo dozi imeisha lakini ile hali ya kuungua ngoz bado inajitokeza naeza lala nikiamka nakuta tayari madoa meusi kwenye miguu ya kuungua naomben msaada jaman
 
Pole sana! Allergy ni hali ya mwili kutoa histamine ambayo huwa antagonist na dawa/kitu ulichomeza. Sasa hali hiyo yaweza kuondoka yenyewe baada ya muda au kutumia dawa sahihi za anti-histamine au dawa za kuondoa sumu ya dawa.

Unashauriwa baada ya kupima na kugundua ugonjwa daktari/mfamasia akupatie dawa (kwa ushirikiano na mgonjwa baada ya kueleza kuwa ana allergy na dawa gani) ambayo ni sahihi kwako. NI HATARI KUMEZA DAWA BILA KUFUATABUSHAURI WA MTAALAMU WA DAWA!

Ushauri: rudi hospitali, elezea historia ya tatizo vzr na kisha utapatiwa tiba sahihi. Zingatia dosage na duration utakayopewa!
 
Inawezekana una aleji na dawa zenye salfa.. nilikua na tatizo kama hilo sasa hivi kila kabla ya kuandikiwa dawa nawaambia nina aleji na salfa so hupewa dawa zisizo na salfa! Imenisaidia sana
 
achana na hizo dawa kabisa na jamii yake yote. ukiumwa malaria tumia ALU.
ni allergic reaction ndio kwa salfa iliyoko kwenye dawa,,,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…