Msaada: Nimeachishwa kazi

likandambwa

Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
18
Reaction score
0
Wasaalam
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza

Niliajiriwa serikali KUU mapema mwaka huu baada ya kusota kwa zaidi ya miaka miwili mtaani katika masharti ya kudumu na mafao ya uzeeni na probation period ya mwaka mmoja

Baada ya miezi 7 tangu nianze kazi niliandikiwa barua ya kuachishwa kazi huku sababu iliyoelezwa ni MISSCONDUCT

lakini kinachoshangaza ni kwamba tangu nianze kazi sikuwahi kuitwa kuhusu shauri lolote linalohusiana na missconduct kati yangu na msimamizi wa kituo cha kazi na nilikuwa nafanya kazi kama kawaida na kiukweli kabisa sikuwahi kufanya kosa lolote lile

Kubwa zaidi nimeandikiwa barua nikiwa katika mapumziko baada ya kumaliza matibabu ambapo yaliyotokana na mimi kupata ajali ya bodaboda wakati natoka kazini ambapo dereva aliingia mtaron na kunisababishia kuvunjika mkono wa kulia ambapo nilipewa rufaa na kuletwa dsm kwa ajili ya matibabu

Baada ya kufanyiwa upasuaji nilirudi kazin (mkoani) na kuwasilisha ED niliypewa na daktari inayonitaka nipumzike kwa wiiki 4 kuuguza mkono

Nimeandikiwa barua ya kuachishwa kazi sku mbili baada ya kuanza mapumziko mara baada ya kurud kutoka kwenye matibabu

Ieleweke kuwa mwajiri wangu yupo dsm na kule mkoani yupo msimamizi

Pia ieleweke nilipewa ruhusa kama kawaida na kupewa fedha za kunisaidia nauli na kujikimu na msimamizi wangu

Nimejaribu kufatilia kupata ufafanuzi nijue makosa niliyofanya lakini mwajiri haoneshi ushirikiano wowote

Je, nichukue hatua gani???

Je, kuna uwezekano wa kurejeshwa kazini?

Naombeni msaada na kama kuna mwanasheria aliye tayari kunisaidia tafadhali, naomba anichek kwa inbox

NB: sijawahi kuitwa kuhsu shauri lolote la maadili au utendajj kazi. Kwa lugha rahsi sjawahi kusikilizwa wala kujitetea

NATANGULIZA SHUKRANI n MBARIKIWE
 
Pole sana mkuu. Makampuni yanatofautiana na sio kila kosa lazima upewe onyo, kuna baadhi ya makosa ukifanya adhabu yake ni kuachishwa kazi japo hilo inabidi liwepo na liwe wazi kwenye mkataba wako wa kazi au kanuni na taratibu za mwenendo wa wafanyakazi wa hiyo kampuni.

Kama haujafanya kosa linaloangukia kwenye hayo yaliyoainishwa ambayo yatakufanya upoteze kazi, unaweza kuanza kutafuta wanasheria kwa msaada zaidi. Kwa kipindi cha miezi 7 kosa pekee ambalo lingekupotezea kazi ni utendaji wa kazi kwa sababu ulikua bado upo kwenye probation, na hapo ungeitwa nakuelezwa ni wapi uongeze bidii ili kuboresha utendaji wako.
 

Asante sana mkuu
Ila sipo kwenye kampuni, hata hvyo sikuwahi kufanya kosa lolote kama nilivyotangulia kusema

Kama nilivyotangulia kusema ni kwamba tangu nianze kazi sijawahi kuitwa kuhusiana na kosa au mwenendo wowote mbaya

Pia kwa mujibu wa mkatab wangu wa kazi ni permenent and pensionable ila kama ambvyo utaratibu wa serikali ningethibitishwa kazini baada ya mwaka mmoja kwisha wa probation

Nashukuru kwa ushauri
 
Mkuu pole sana

Mimi hua naamini kila tatizo linalonikuta ni kwasababu MUNGU anajua mimi ndiye nitakayeweza kulihimili

Amini hivyo na kulingana na dini yako MUNGU atatenda!

Amen!! Asante sana kaka
 
Kama umepewa barua ni lazima imetaja na sababu ya kuachishwa kazi na ni lazima itakuwa imetoa maelekezo ya nini ukifanye kama hukuridhika na uamuzi huo.

Nenda kwenye chama cha wafanyakazi unachochangia ukiwa na salary slip yako haraka sana maana kwenye mambi kama hayo ishu ya muda ni relevant.
 

Nimekuelewa ndugu yangu, hata kama ni serikalini lazima kuna taratibu zinazosimamia mwenendo na utendaji wa wafanyakazi hapo ofisini.
kwa mujibu wa maelezo yako, umeonewa tusubiri msaada kwa wataalam wa sheria japo Watu8 anaweza kutoa ushauri wa wapi pa kuanzia.

shukran
 
Last edited by a moderator:
Mkuu usikubali ipoteza haki ako kuna taasisi nyingi tu zinasimamia haki za wafanyakazi embu anza nazo hizoo utapata msaada serikalini alaf unafukuzwaje kazi kienyeji hivyoo mkuu naamini utapata haki yako tu
 

Mkuu kiukweli nimeambiwa tu ni MISSCONDUCT though sjui ni missconduct gan
Na wala barua haijaeleza kama sijaridhika nifanye nn

Ni kwamba nimeambiwa tu nalipwa mshahara wa mwezi mmoja badala ya notice

Kuhusu suala la chama cha wafanyakazi to be honest.. Nilikuwa sijajiunga bado
 
Mkuu usikubali ipoteza haki ako kuna taasisi nyingi tu zinasimamia haki za wafanyakazi embu anza nazo hizoo utapata msaada serikalini alaf unafukuzwaje kazi kienyeji hivyoo mkuu naamini utapata haki yako tu

Kama taasisi gani mkuu tueleweshane nahitaji msaada kweli
 
Ww unazingua, ulikuwa kwenye probation ukachukua leave ukute ulisingizia ugonjwa, nnavojua ukiwa kwenye probation yo nat etittld kuchukua leave, kama kwel ulikuwa waumwa bas umeonewa bt kama ulfanya ubishooo ili ule bata imekula kwako
 
Kaka maelezo yako yenyewe yanajikangana,bt sema upo serikali kuu au za mitaa au shirika la umma tuangalie jinsi ya kukusaidia.
Alafu toa information vzr na zote ilivyo tokea muda huu siyo mda wa kuficha chochote.usipokuwa makini hyo kazi utapoteza mazima.
Alafu jua huwa si rahisi kufukuzwa kazi serikalini lazima kuna vikao kama 3 viwe vimefanyika juu yako na bado wanakupa muda wa kukata rufaa.pia barua huwa inaelewa kuwa kutokana na kikao cha tarehe fulani..bodi ya ajira imekufukuza kazi kwa sababu hizi ! Pia kabla ya hapo na wewe lazima utakuwa umepewa nafasi ya kujitetea mbele ya bodi.
 
Ww unazingua, ulikuwa kwenye probation ukachukua leave ukute ulisingizia ugonjwa, nnavojua ukiwa kwenye probation yo nat etittld kuchukua leave, kama kwel ulikuwa waumwa bas umeonewa bt kama ulfanya ubishooo ili ule bata imekula kwako

Mkuu hakuna ubishoo hapa
Nilivunjika mkono baada ya kupata ajali ya bodaboda wakati narud nyumbani kutoka kazini ambapo dreva aliongia mtaron nikarushwa

Nikaletwa dsm kwa ajili ya matibabu baada ya kupewa rufaa

Baada ya kufanyiwa opereshen nikapewa E.D ya wiki nne na ukizingatia mkono uliovunjika ni wa kulia kwa hyo haufanyi kazi vema

Nilivyorud kwa msimamizi wangu nikawasilisha ED lakn after 2 days nikaletewa barua ya kuachishwa kazi kutoka kwa mwajiri dsm

NB
IELEWEKE KUWA NINAFANYA KAZ MKOAN NA MWAJIRI YUPO DSM
HUKU KUNA MSIMAMIZI TU
 
mkuu pole sana .

kwanza naomba udonlod Employment and labour relation act ya mwaka 2004

alafu pitia vifungu vifuatavo kwa vile umenambia unafanya seriklini.


emploiment standads . section 14 hadi 16 kwa umakini mkubwa

alafu soma ukizidisha uumakini mara mbili sub part e (unfair termination) inapatkana section 35 hadi section 44.

baada ya kuelewa hapo soma section 32 inaelezea mambo ya sick leave na mambo ya gonjwa kazini.

katika jinsi yakutatua mgogoro wako kuna hatua ya cma imeelezwa section 86 kuendelea

ikishindikana hatua hiyo maahakama itausika na mahakama itaamua vitu vitatu reingejiment kompasesheni au riinstetment. kwa mujibu wa section 40.




haya yote yatawezekana kama umefanya kazi zaidi ya miezi sita .


ikiwa ndivyo soma uelewe kesi umeshinda komaaa
 

Mkuu huo ndo mtiririko halisi wa jambo lilivyotokea

Mkanganyiko unaouona ww nami nauona hvyohvyo ndo imeniacha mdomo wazi
 
kwa kuongeza kwa mujibu wa sheria hairuhusiwa kumfukuza kazi mtu akiwa likizo katika mazingira yeyote ile.pia iyo section 35 inaeleza jinsi na makosa ya kufukuzwa kazi ikiwemo prosija ,tafadhali soma uelewe ivo vifungu then utafte msaada wa kisheria serikali inafanya kazi chini ya iyo sheria mama ya kazi,kila la heri mkuuuu.
 

Kuwa makini inawezekana msimamizi wako amekuchongea kwa mwajiri wako ndio maana ukalimwa barua ya kupoteza kazi.

Who knows bana binadamu hatupendani hasa katika maeneo ya ajira.
 
Hapo kuna mchezo mchafu umefanyika ambao msimamizi wake anataka kumuweka mbadala wake!So that is very bad ila kama ameeleza kweli,hakika atarudi kazini!
 
Kuwa makini inawezekana msimamizi wako amekuchongea kwa mwajiri wako ndio maana ukalimwa barua ya kupoteza kazi.

Who knows bana binadamu hatupendani hasa katika maeneo ya ajira.

Hata mimi nahisi hivyo mkuu na hata wafanyakaz wengne wanashangaa na wanamhsi msimamizi ndo kafanya hvyo maana wanasema ndo zake hasa ukizingatia nilikuwa kwenye kitengo cha karibu na yy kama msaidizi wa karibu katika masuala ya management

Pamoja na hayo je nichukue hatua gan mkuu
 
Hapo kuna mchezo mchafu umefanyika ambao msimamizi wake anataka kumuweka mbadala wake!So that is very bad ila kama ameeleza kweli,hakika atarudi kazini!

Je nichukue hatua gan? Maelezo niliyotoa ni ukweli mtupu na sina sababu ya kuficha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…