Msaada: Nimefanya kazi miezi 3 mwajiri hataki kunipa mkataba

thomas_360

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2015
Posts
1,458
Reaction score
1,432
Nawasalimia wakuu wa jf..Mimi nikijana ambaye nimehitimu mwaka huu kwenye chuo fulani hapa tanzania, kunasehemu nilipata nafasi ya kufanya kazi ila nilipewa muda wa miezi mitatu ya majaribio, baada ya hapo ningepewa mkataba.

Muda wa miezi mitatu umeshafika na mwajiri wangu haoneshi uelekeo wa kutoa mkataba na ukiangalia pesa yenyewe napewa kidogo. Ni kampuni moja ya wahindi ipo dodoma. Hivyo nataka kujua kwa hali kama hiyo napaswa kufanyaje?
 
Kiaheria unapokuwa kwenye majaribio huwa tunasema upo probation period na ikiisha inatakiwa mwajiro either ku confirm au kuto confirm mkataba wa kudumu. Kama umeendelea kupiga kazi kitaalama tunaweza ki draw inference kwamba umefanya kitu kitaalam kinaitwa contract by default. Ila ni muhim kuulizia status ya mkataba wako ili upate na mshahara wa mwajiriwa wa kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…