Msaada: Nimefikia hatua ya kunywa Pepsi 4 kwa siku, nifanyeje kuacha?

Miss_Mariaah

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
2,176
Reaction score
4,979
Habarini za mchana,

Wakuu mimi huwa situmii pombe, ni juice na soda tu na soda yangu pendwa ni Pepsi.

Kila siku huwa nakunywa Pepsi tena napenda ikiwa baridi sana. Nilianza kunywa moja kwa siku, ikaja mbili ikaja 3 now nakunywa nne kwa siku; mbili mchana na mbili usiku. Hizo mbili nakunywa kwa mpigo.

Nifanyeje ili kuacha? Pia Mimi sio mpenz wa chai asubuhi, niko radhi nile vitafunwa vikavu au na maji au soda, na usiku siwezi kulala bila kunywa maji baridi-huwa nalala na jug la maji pembeni.

Nikinywa maji baridi akili huwa inarelax, nalala kwa haraka tofaut na nisipokunywa maji. Nifanyeje?
 
Anza kupunguza. Kama hizo mbili za usiku unakunywa nyumbani usinunue kabisa. Fridge lako lijae maji. Na mchana kunywa moja tu. Jizoeshe kutembea na chupa ndogo ya maji uwe unakunywa badala ya Pepsi.
 
hio haiko sawa, ngoja madaktari waje wakueleze lakini why usiwe unatengeneza juice natural ikawa ndio fav yako mbadala wa hio pepsi?
hio haiko sawa, ngoja madaktari waje wakueleze lakini why usiwe unatengeneza juice natural ikawa ndio fav yako mbadala wa hio pepsi?
Hua natengeneza ila Pepsi Iko tofaut na juice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…