Msaada: Nimetumiwa ujumbe huu

mrm

Member
Joined
Dec 16, 2014
Posts
24
Reaction score
8
Habari wana Jf,, kuna rafiki yangu amenitumia textmessage' hii nanukuu: "Kuna mtu amenipigia simu anaitwa Abdala Tito eti anasema kesho niende kwenye usahili posta (dar) UTUMISHI wanatoa ajira kwa watu maalum (ambao ni walimu 'graduates' ambao wataajiriwa kama watumishi ktk idara ya elimu lakin si kufundisha mashulen) tu nami ni mmoja wao. Wewe umeusikia utapeli huu au ni kweli? Mimi sijamuamini hata kidogo japo anajibu maswali vizuri kweli utadhani ndio utaratibu mpya.Najua serikali haiwezi kufanya mambo hivyo". Mwisho wa kunukuu.

Nimekosa cha kumjibu kwasababu sina ufahamu katika hilo. Hivyo ninaomba mnisaidie hii kitu ni kweli ipo au kuna kamchezo kanakofanywa na huyu bwana Abdalla Tito?.
 
Usaili posta? halafu ana uzoefu kwa kiasi gani mpaka atoke chuo na moja kwa moja akawe mtumishi wizarani? Na pia wizara shughuli zake nyingi zinafanywa Dodoma iweje aitwe posta kwenye majengo marefu na mjini kiasi kile! Asijaribu kwenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…