Jamani hodi!
Wanajamvi sote tunafahamu hali ya uchumi ilivyo. Nisaidieni mawazo nimetapeliwa, ilikuwa hivi:
Kuna dogo tuliongea biashara ya dagaa, akaniambia dagaa wanalipa ila mtaji tu ndio hana. Basi mimi nikamtathmini nikamuona ni dogo fighter, nikaona nishirikiane nae kwa masharti nafuu ili hata yeye anufaike, kiroho safi kabisa.
Basi nikamwambie tufanye hiyo biashara mimi nitoe mtaji na yeye ndio apige kazi then analeta mahesabu kila baada ya siku mbili tunagawana faida 50/50 mtaji unabakia kuwa mali yangu.
Nikiamini kuwa mwisho wa siku naye atakuwa na mtaji wake. Dogo alionekana mstaarabu sana na ana sifa zote, nami nilimkarimu kwa kila hali ili afanye kazi akiwa stress free.
Nikampa kwanza laki tano za kuanzia tuone biashara onavyojwenda, kweli mwanzoni akawa analeta faida vizuri, kisha analangua mzigo tena anauingiza sokoni, alileta mahesabu wiki mbili bila taabu yoyote na biashara ikawa inaenda vizuri.
Baadae akaja na hoja kuwa kuna dagaa wa grade ya juu anashindwa kuwanunua kwa kuwa mtaji ni mdogo kama inawezekana nimwongezee laki nne ili awe ananunua walao wa grade tatu tofauti ili kupanua wigo wa wateja.
Mimi kwakuwa nilishaonjeshwa faida nzuri nikasema wacha nijilipue basi nikapambana baada ya siku mbili nikamrushia zile laki nne.
Hapo sasa tayari ana pesa yangu laki tisa. (Kumbuka makubaliano ni kugawana faida, mtaji ni wangu, mwisho wa siku mtaji unatakiwa urudi kwangu).
Basi dogo tangu nilipomtumia ile laki nne hataki kuleta mahesabu, zaidi ananambia alinunua mzigo umemkata, ananiambia ananutafutia hela yangu anirudishie.
Nikimwambia njoo basi home tuongee ana kwa ana unieleze imekuwaje, hataki.
Nimechanganyikiwa kiukweli. Mimi nadunduliza kwenye kibarua changu hadi nikapata hiyo pesa nilompa nikiwaza nini kujiongezea kipato, sasa badala ya kuinuka ndio nimedidimizwa, halafu ni kabwana mdogo tu.
Jamani tuache masihara sili sipati usingizi, nimfanyeje huyu dogo? Je, nimpelekee polisi nimsweke ndani kwa siku kadhaa? Au nimfanyeje? Sio siri napata mawaza mabaya sana juu yake. Msaada wana jamvi.
Pesa nilikuwa namtumia kwa M-Pesa na miamala yote na mawasiliano yote ninayo kwenye simu yangu.
Nimefuatilia sokoni yupo na anaendelea kupiga kazi. Msaada jamani kabla sijaleta balaa!