Msaada: Nimjamzito lakini naona damu

reen elius em

Member
Joined
May 17, 2014
Posts
56
Reaction score
5
Habarini ndugu zangu,

Mimi nina mimba ya mwezi mmoja lakin kuna utofaut niliona,nilianza kuumwa sana tumbo gafla afu damu zikaanza kunitoka.

Lakini nikaulza nilijibiwa ni kawaida damu inaeza kutoka kidogo wakati una mimba.

Cha ajabu damu ziliendelea kutoka kwa mda wa wiki nzima yani kama nmeingia hedhi na tumbo linauma,mwisho damu zikakata.

Kuna rafiki yangu nikamhadithia kilichontokea akadai ni tatizo, nikanunua kipimo nilipopima nikakuta mistari miwili mmoja uko wa mbali mno yani wakati nilipopma mara ya kwanza ilikua yote inaonekana mistari miwili.

Jamani nisaidien ni hali ya kawaida tu au ni tatizo?
 
wakati mwingine ukiona shida kwa hali hiyo nenda hospital achana na ushauri wa mtaani. hiyo mimba inakuwa imeharibika lakini ungewahi hospital ungesaidiwa
 

mstar wa pili ukiwa umefifia t meanz mimba changa...nenda hosptal kapge ultra sound wataona..ondoa hofu tu
 
Naungana na wanaokwambia uende hospitali,nami nakushauri hivyohivyo.
 
Pole..maana sio dalili nzuri kusema ukweli..kama utakua salama basi siku jiepushe kufanya kazi nzito kama kubeba ndoo za maji.. mizigo mizito..kazi ngumu n.k..
 
Pia ukiwa unafanya kazi sana uwa inatokea sana but nenda hospital ndio utapata jibu la uakika...pole sana Mungu akuponye
 

tatizo kama hilo mdada anzia kwanza hospitali halafu ndio uje humu kupata experience toka kwa watu wengine.

au ikishindikana hospital ndio uje kuuliza humu.
 
Nenda Kituo cha afya Mapema usisubiri majibu ya Wapita njia. Afya yako ni Muhimu sana kwa Kizazi chako na wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…