Msaada: Nina Funza Mguuni

Heisenberg

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2017
Posts
1,691
Reaction score
2,967
Kwanza Niungane na Muhenga Aliyetunga Methali isemayo " Mficha Maradhi Kifo humuumbua"
Na kwa sababu sitaki kifo, nimekuja kwenu kuomba msaada.

Wakuu naandika Thread hii ikiwa ni Saa 9 usiku baada ya kukosa usingizi kabisa licha ya kuwa na uchovu wa wiki nzima inayoishia.
Nimeshituka saa 8 za usiku na kukuta mguu unawasha Sana ila ni maumivu ambayo sometime yanaambatana na Utamu fulani hiviiii
Nikaanza kujikuna, lakini maumivu ndo yanaongezeka kiasi kwamba inabidi nijikune Throughout.

Ki ukweli mimi Naishi Moshi. Nipo kwa Muda sasa maeneo haya na eneo hili lina vumbi sanaa. Imebidi nimuulize jamaa yangu usiku huuu kuwa hili ni tatizo gani??

Amenijibu kuwa ni Funza. Sasa mimi sijui hata hawa funza wapoje. Si unajua tena sisi Watoto wa Das'lam hivi ni vitu vigeni kwetu.

Hivyo wakuuu naomba ABC za kufanya utatuzi wa hili suala maana shidaaaaaaa.
Yani nimekosa amani kabisa.
Pia naomba na njia za kujikinga na janga hilii
 
Tafuta oil chafu upake pale juu ya funza kila siku usiku funza litakosa hewa na kuozea mumo kwa mumo na utapona bila hata kulitoa. Pia ukikosa oil chafu paka hata mafuta ya mgando it may help sababu dhumuni ni kulinyima oxygen lifie mumo kwa mumo.
 
Tafuta oil chafu upake pale juu ya funza kila siku usiku funza litakosa hewa na kuozea mumo kwa mumo na utapona bila hata kulitoa. Pia ukikosa oil chafu paka hata mafuta ya mgando it may help sababu dhumuni ni kulinyima oxygen lifie mumo kwa mumo.
Dawa ni kumtoa tu.
Atumie pini au sindano ya kushonea nguo amng'oe then apake mafuta ya taa kuua mayai au masalia yake kama yatabaki.

Pia mafuta ya taa yanaua huyo kiumbe ukiweka na chumvi
 
Watu wengine mnajua 'kufake' kwa kweli. Na ndio uanaume wa Dar huo.

Yani upo na mtu ambae ameweza kujua tatizo ni funza alafu huyo mtu asikupe suluhu ya tatizo hilo mpaka ulete uzi JF?

Nadhani umetumia akili za huyo funza aliyeko mwilini mwako.
Boss sisi huku wote ni wa kuja tuuu. Hata mm nilijua ni funza ila nilikuwa nataka confirmation. Vipi Songea wazima??
 
Pole sana mkuu,mwagia mafuta ya petrol sehemu alipo huyo bwana funza then pitisha moto hiyo sehemu.
 
Kata mguu huo mkuu. Uspoangalia atakusababishia kansa ya damu
 
Nenda hosptal
 
Kimbia KCMC mkuu. Utafanyiwa ct scan kujua ni funza gani. Wahi usije katwa mguu.
 
Muulize tiba huyo uliyenaye,si yeye ni mwenyeji wa hukohuko.
 
Wakuu nimepata tiba. Mwenyeji ametumia Sindano kumtoa na akanipaka mafuta ya taa sasa hivi niko poa sana asanteni kwa michango yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…