MSAADA;NINA mil.3,NATAKA KUWEKA DUKA.

MSAADA;NINA mil.3,NATAKA KUWEKA DUKA.

Fungo N.

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
252
Reaction score
43
Wana jf,nipo chalinze,nina kiasi cha Mil.3,ninataka kuweka duka hapa,ila sina uzoefu na biashara hii.LAKINI pia nimewaza kuwa pengine kiasi hicho nifungue saloon ya kiume au kike.USHAUR TAFADHALI
 
kama ni za uridhi utajiua siku sio nyingi Biashara ina wenyewe na ukitaka kudumbukiza zote zitaisha zote ,Mvua zinachanganya sana sasa hivi tafuta heka nne ulime mahindi gharama itakuwa kama milioni hivi mpaka kuvuna utauza na kupata milioni nne au tano,utalima tena na kupata mara mbili huku ukiwa na akiba yako benki unaanzia hapo kuuliza habari za duka sasa hivi labda MPESA au saloon ya kiume
 
Mkuu mbona unakatisha watu tamaa kiasi hicho? Kufeli kuko kila mahali hata kama nikazini unaweza fukuzwa tu, so si vizuri kumvunja mru moyo kiasi hicho
 
Uoga wako umasikini wako...vijana wengi wanaogopa kujaribu...jaribu tu kaka wawezafungua duka..ukishaingia kwenye biashara utajifunza mengi zaidi...try
 
Wana jf,nipo chalinze,nina kiasi cha Mil.3,ninataka kuweka duka hapa,ila sina uzoefu na biashara hii.LAKINI pia nimewaza kuwa pengine kiasi hicho nifungue saloon ya kiume au kike.USHAUR TAFADHALI

daa.. huu mwezi wa Januari ni mwezi dume kweli kweli. sasa Fungo N. wakati unasubiri upate ushauri muafaka wa wana-JF nakushauri nikutunzie hizo pesa. nikupe namba yangu ya MPesa au akaunti yangu ya CRDB? usikurupuke kufanya biashara bila kuielewa kwa undani...utaipoteza hiyo 3m. yako. subiri watalaam wa biashara humu JF watakupa ushauri.
 
Anza kidogo tumia kama nusu ya mtaji wako kwanza, hapa siyo suala la uoga bali ni mkakati tu huu! Hii awamu ya kwanza usilenge zaidi kupata faida bali tumia fursa hii kujifunza zaidi kwako mwenyewe na kwa wengine wanaofanya hiyo biashara! Utakapoianza wewe utakuwa ni mwanafunzi tu kwa hiyo usifanye kihelehele cha kumwaga mtaji wote! Jifunze kwanza mikwara ya hiyo biashara, kuna tuvitu tudogo tudogo hatuandikiki hapa utatugundua na ukishaijua njia zake sawasawa sasa hapo kanyaga twende kwanguvu zote! Ukianguka usikimbie endelea kujiboresha, jifunze kwa waliofanikiwa utawakuta tu! Au la kaombe kazi ya kuuza duka la mtu kwanza upate shule ya bure! Mtaji mkubwa wa kwanza ni ujuaji wa jinsi ya kuendesha duka!
 
kwanza tafuta location nzuri kwa ajili ya biashara yako. Pia tambia mahitaji wa wateja wako. tatu, uwe na kauli nzuri kwa wateja. Nne, kwa vile mtaji wako ni mdogo basi anza kidogo kidogo huku ukisoma biashara yako na kujifunza zaid. Ukipata uzoefu anza kuipanua biashara yako taratibu. Zaidi ya yote simamia biashara yako wewe mwenyewe kama huna majukumu mengine ila kama una majukumu mengine basi tafuta mtu mwaminifu auze duka lako ingawa watz waminifu ni wachache sana.
 
Wana jf,nipo chalinze,nina kiasi cha Mil.3,ninataka kuweka duka hapa,ila sina uzoefu na biashara hii.LAKINI pia nimewaza kuwa pengine kiasi hicho nifungue saloon ya kiume au kike.USHAUR TAFADHALI

watu tutakuja humu na mawazo mbalimbali jitahidi kuzingatia yale ya upande chanya,tafuta biashara itakayoendana na eneo lako kwa sababu biashara inataka uzoefu kama kitu kingine chocho kile usiweke hela yote kwaa kuanzia,anza na hela kidogo kadiri uzoefu na mtaji utavyoenndele kukua,ukiona kuna ugumu sana na matatizo yanaongezeka na wewe ndio uongeze nguvu maana yake unakuwa unakaribia kufanikiwa, "kukikiwa na mvua kubwa storm huwa inaanza then kunakuwa shawri"all ze best
 
Nashukuru,hope kufikia mwz june 2013 nitakupa feedback
 
Wana jf,nipo chalinze,nina kiasi cha Mil.3,ninataka kuweka duka hapa,ila sina uzoefu na biashara hii.LAKINI pia nimewaza kuwa pengine kiasi hicho nifungue saloon ya kiume au kike.USHAUR TAFADHALI

Jiulize kwa nini duka? duka la nini? eneo unalotaka kufungua kuna maduka mangapi kama hilo? wateja wapo? malighafi (vifaa vya dukani) kwa jumla vinapatikana kirahisi? muuzaji mzuri unaye? mshahara wake je? (hata kama ni wewe mwenyewe lazima ujilipe); usisahau pesa ya pango, leseni na kodi nyingine kama ulinzi n.k.

Si vibaya ukitembelea maduka ya jumla ili kujua bei ya bidhaa kwa lengo la kujipanga ni bidhaa gani inayotembea na kufanya mzunguko mzuri. Usiogope; jipange vizuri na kila kitu kitaenda salama. Nakuaminia Mkinga wewe!
 
Hapo kwenye saloon ya kiume tupo wengi,mzoefu atuelezee vizuri jamani kwa mazingira ya geita mjini.
 
Back
Top Bottom