Mkuu zipo biashara nyingi saana za kufanya
Kitakacho determine ufanye nini inategemea na mtaji,mahali unapoishi, interest, muda wako utakaowekeza kwenye hiyo biashara-Kumbuka kama wewe ni muajiriwa kuna baadhi ya biashara zitakushinda mfano kutoa bidhaa hapo kigoma na kupeleka mikoa mingine,
Chakufanya pitia hili jukwaa kuna MADA ya member moja anaitwa MBU- isome kuna michango mizuri saana, kuna mada za ufugaji wa kuku-wa kisasa na kienyeji, ukizisoma zote ka makini hutatoka kapa
Cha msingi huo mtaji ulionao unatosha kabisa kuongeza kipato, anza kuangalia mazingira unayoishi lazima kutakuwa na opportunities kibao, angalia watu wanakula nini, wanakunjwa nini, kipato chao, aina ya maisha watu wanayoishi,mila na desturi, ukiyafanyia kazi yote hayo naamini lazima utapata idea ya ni biashara gani ya kufanya. angalia kama ijumaa na jumamosi kunakuwaga na harusi nyingi- unaweza anzisha kabiashara ka upambaji, kama hakuna maduka ya vyakula unaweza fungua retail shop, kama kuna baa unaweza fikiria vinjwaji vya jumla na rejareja..
pia unaweza fikiria biashara ya ngua,,unaweza uza nguo za watoto, vijana, mali unaweza pata kariakoo kwa bei rahisi tu... ukishindwa yote hayo nunua pikipiki
kila la kheri