MSAADA: Nina tatizo la kuumwa tumbo muda wote iwe nimekula au sijala

Joined
Dec 27, 2018
Posts
12
Reaction score
2
Wasalam wadau,
Nina tatizo la kuumwa tumbo muda wote iwe nimekula au sijala.

Lilianza mwaka 2009,nilipoenda hospital nikafanya kipimo kinaitwa barium meal nikaelezwa nina vidonda vya tumbo,nikapewa dawa lakini hazikusaidia,nikahamia tiba mbadala haikusaidia.

Mwaka huu nimefanya kipimo cha OGD zaid ya mara nne nimeambiwa sina vidonda lakin tumbo linauma tu,
1.kuna muda linawaka moto
2.kuna muda linakwangua
3.kuna muda linajaa gesi
4.kuna muda linavimba
Na hayo maumivu ni hapa juu ya kitovu.
Msaada tafadhal,,kama kuna mwenye experience na hili.
 
Huwa unakunywa soda/juice za dukani nk?
 
Njoo inbox, nikushauri kitu kwa simu
 
Dalili za ulcers hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kukiwa na chakula tumboni, huwa unaendelea kuhisi linakwangua na kukuunguza? inaelekea una active peptic ulcers... ila nijibu ilo swali kwanza then nikupe ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokana na tatizo lako, kuna vyakula unatakiwa usivitumie. Vyakula vyenye asidi kali jamii ya machungwa(limao,ndimu n.k), pilipili,maharage n.k unatakiwa uviepuka itasaidia kupungua kwa maumivu kwa kiasi flan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ni dalili za ulcers! Chakufanya nenda kapime
H -Pylori
Usile vyakula Vya kukaanga kwenye mafuta maana vinaongeza ACID! Hivyo ni pamoja na Nyama choma, chips mishkaki nk

Achana na Vyakula vyenye ndimu au pilipili!

Epuka vyakula vyenye acid kama vile soda na vinywaji Vya kuongeza nguvu nk

Jitahidi usishinde na njaa
 
Kipimo cha OGD hakikuonyesha vidonda
Uko wapi na hicho kipimo ulipima wapi? Na baada ya kuambiwa sio vidonda walichukua hatua gani au wewe mwenyewe ulichukua hatua gani.
Maana hauwezi kuambia tatizo halijulikani halafu ukaridhika, kwanza hakuna Dokta wa hivyo. Vipimo vyote hivyo kutoonesha tatizo angeenda next step hata biopsy angechukua unless wewe wenyewe ndio haukuwa tayari kuendelea na matibabu, maana wakati mwingine sisi wenyewe tunaoumwa ndio huwa tunakuwa kikwazo cha matibabu kwa kutokumpa Dr muda.

Upo mkoa gani mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…