illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
naomeni msaada wa kisheria ili nijue pa kuanzia, mume wangu alifanikiwa kuanzisha kampuni kwa kushirikiana na raia wa kigeni mwaka 1998 ambapo alikuwa ni mwana hisa, mmoja wa wakurugenzi bahati mbaya mwaka huo huo alifariki, kwa uelewa wangu mdogo nimekuwa nikienda pale kwenye kampuni kuulizia hatma ya hisa au gawio. kwani kikao cha familia kilijadili na kuniteua kuwa msimamizi wa mali za marehemu lakini nimekuwa nikipata ushirikiano hafifu na vitisho, wamekuwa wakiniambia kuwa haya mambo yamekaa kisheria zaidi na kama unaouwezo nenda mahakamani, nimeulizia taratibu za mahakama ni mpaka uwe na mwanasheria ambapo ni gharama kubwa nisizoweza kuzimudu niliwahi kwenda brela mwaka jana 2015 nikakuta bado wanaendelea kulitumia jina la marehemu mume wangu kama miongoni wa wanahisa hivyo katika taarifa zao za kifedha inaonyesha kuwa bado anapata gawio..shida yangu kuu ni kuweza kutoa mtaji ama hisa alizoweka wakati wa kuanzisha kampuni pili kupata gawio la muda wote ambao wamekuwa wakilitumia jina la marehemu kama miongoni mwa wanahisa ....tatizo ni kwamba gharama za kuendesha kesi siwezi kuzimudu msaada wowote utashukuriwa sana