MSAADA:NINI MAANA YA UVUMBA?

MSAADA:NINI MAANA YA UVUMBA?

Full charge

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2018
Posts
1,678
Reaction score
1,617
Kama kichwa cha habari kinaonesha,naomba wajuvi wa Kiswahili wanisaidie.
 
Kama kichwa cha habari kinaonesha,naomba wajuvi wa Kiswahili wanisaidie.
Neno hilo linaweza kumaanisha moshi au ubani unaochomwa. Hutengenezwa na manemane yenye harufu nzuri na gundi, kama vile ubani na zeri. Vitu hivyo hupondwapondwa na mara nyingi huchanganywa na vitu kama vile viungo, magamba ya miti, na maua ili kutengeneza aina mbalimbali ya manukato kwa makusudi hususa.

Uvumba ulipendwa sana na hivyo ukawa bidhaa yenye thamani sana nyakati za kale na viungo vyake vikawa muhimu katika biashara. Misafara ya wafanyabiashara ilileta ubani kutoka nchi za mbali. Huenda ukakumbuka kwamba Yosefu, mwana mdogo wa Yakobo aliuzwa kwa wafanyabiashara Waishmaeli waliokuwa ‘wakija kutoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri.’ (Mwanzo 37:25) Watu walitaka sana ubani hivi kwamba njia iliyoanzishwa na wafanyabiashara wa ubani ilitumiwa kusafiri kati ya Asia na Ulaya.

Dini nyingi leo zingali zinafukiza uvumba katika sherehe na desturi zao. Zaidi ya hayo, watu wengi hupenda kufukiza ubani nyumbani mwao ili kufurahia tu harufu yake nzuri.
 
Back
Top Bottom