msaada tafadhari usingizi nimekuwa nikipata kwa masaa machache mno tofauti na awali.
Pole sana!
Kukosa usingizi (insomnia) ni tatizo la afya ya akili ambalo lina visababishi vingi mfano
-kelele nyingi ktk mazingira unapolala au wakati wa kulala
-hali mbaya ya hewa hasa joto
-mfadhaiko (stress)
-maumivu
-matumizi ya dawa/madawa, pombe
-ulaji au aina ya vyakula na muda wa kula na muda wa kulala
-msongo wa mawazo (depression)
-matatizo mengine ya afya ya akili nk
Kitaalamu mtu mzima hutakiwa kulala kwa walau saa 7.5 hadi 8 kwa usiku. Hata hivyo kuna baadhi ya watu hulala kwa saa 3 tu lakini hawapati shida yoyote.
Ili kutibu insomnia jambo la kwanza ni kutafuta kisababishi na kukishughulikia. Pia kama mtu hulala saa chache lakini haimuathiri ktk shughuliki zake za uzalishaji hakuna haja ya matibabu, tiba ni kwa yule ambaye kutokana na kukosa usingizi (insomnia) na wanapoamka hushindwa kufanya shughuli zao za kawaida kutokana na uchovu.
Tunashauri kuepuka ktumia baadhi ya dawa ili kupata usingizi bila kujua chanzo cha kukosa usingizi (insomnia). Hii ni kwa sababu unaweza kupata utegemezi kwa hizo dawa ili kuweza kulala ( dependence) kwani hujatibu chanzo.
Kwa hiyo angalia mtindo wako wote wa maisha kama kuna vitu vipya, epuka kuingia kitandani kulala muda mfupi baada ya kula, fanya mazoezi na epuka visababishi kama utabaini. Lakini nakushauri ufike hospital ili uonane na daktari kwa uchunguzi, ushauri na matibabu zaidi.
Pole sana!