Msaada: Nipate wapi mkopo wa milioni 20?

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,327
Reaction score
4,624
Wasalaam!

Mimi ni mwajiriwa wa taasisi fulani binafsi. Nina mshahara take home zaidi ya millioni 2.5. Ninatafuta kiasi cha sh. Million 20-25 ili kununua uwanja.

Nimeshindwa kukopa benki za biashara kwa sababu mwajiri wangu hayuko tayari kunidhamini, na hata benki zikija ofisini hukataa kujenga mahusiano nazo.

Wapi naweza pata msaada? Niko radhi nikatwe kati ya milioni moja hadi milioni moja na nusu kwa mwezi.

Wakatabahu
 

Kwa Pesa unayoipata kwa mwezi ungeweza ku~save' kama m2 kwa mwezi.Ukala laki 5 ila hapa cjui mtimdo wako wa maisha na matumizi yako kwa mwezi.Hivyo ungeweza kutengeneza m20 ndani ya miezi 10 tu na kuendelea na wazo lako la biashara kwa uhakika.Hii pia itakujengea uwezo wa ku~save na kujiwekea malengo.

Kuhusu wapi kwa kukopa?
1:Kwa aina ya mwajiri uliye naye huna njia nyingine isipokuwa kujiunga na SACCOS kama WAT SACOS kwa Dar,sijajua wewe uko wapi.Ila nao wana utaratibu wao ikiwepo kujiwekea akiba kiasi walau 1/3 ya mkopo uutakao ili kukuwezesha kukopa mara 3 ya akiba uliyonayo.

2:Unaweza kuomba uiingiziwe mshahara wako kwenye Benki zinazotoa mikopo kwa waajiriwa kama Baclays.

3:Tembelea taasisi zinazotoa mikopo kwa wajasiriamali kama EFC na nyinginezo.
All the Best.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…