Najua humu ndani naweza kupata msaada wa namna ya kudai mishahara yangu iliyozuiliwa kwa muda wa miezi nane huku nikiendelea na kazi.
Mshahara wangu ulizuiliwa baada ya kutokuwepo kazini kutokana na kuugua wakati wa likizo. Baada ya kupona, nilirejea kazini na kuwasilisha ushahidi wa kidaktari kuthibitisha kuwa nilikuwa naumwa. Waliporidhika na ushahidi huo, wakanirudisha kazini. Hata hivyo, ilichukua miezi nane bila mshahara wangu kurejea. Baada ya miezi hiyo, mshahara ulianza tena kama kawaida. Nilielekezwa kuandika barua ya kudai mishahara ya miezi hiyo nane. Baada ya kuandika barua na kujaza fomu maalumu ya kudai malimbikizo (arrears), kila ninapokwenda kwa HR kuulizia, wanadai kazi yao ilishakamilika na malipo yapo mikononi mwa Hazina.
Nashindwa kuelewa hatua nyingine za kuchukua kwani mtu pekee ninaweza kumuulizia ni DHRO.
Nifanye nini? Na ni mbinu gani naweza kutumia, kwani pia kuna mishahara ya miezi ya mwanzo wa ajira yangu ambayo sijawahi kulipwa hadi leo.
Naomba msaada wenu. 🙏