chukua huu ushauri,kingine hiyo hela usiitegemee sana.Mkuu kama kweli hao utumishi walisha wasilisha nyaraka zako kunakohusika, subiri utalipwa tu. Malipo ya serikali Huwa hayapo fasta fasta kama kama unavyo tarajia. Hayo malipo yanaweza kuchukua hata miaka 3 kupata hiyo pesa Yako.
Duh, no wonder inflation will never stop...Hizo siku 123 umezitoa wapi mkuu!?,Mimi najua standing order inasema ni miezi 6 full payment,na baada ya hapo 6 months half payment na baada ya hapo tena unasitaafishwa
Ongea vizuri na afisa utumishi anayehusika na payroll hapo halmashauri kwako! Hao jamaa wanafahamiana na jamaa walioko hazina, mbona fasta tu! Wacha ubahiri kijana vinginevyo utakaa mpaka uchaguzi wa 2030 ndipo utalipwa!Najua humu ndani naweza kupata msaada wa namna ya kudai mishahara yangu iliyozuiliwa kwa muda wa miezi nane huku nikiendelea na kazi.
Mshahara wangu ulizuiliwa baada ya kutokuwepo kazini kutokana na kuugua wakati wa likizo. Baada ya kupona, nilirejea kazini na kuwasilisha ushahidi wa kidaktari kuthibitisha kuwa nilikuwa naumwa. Waliporidhika na ushahidi huo, wakanirudisha kazini. Hata hivyo, ilichukua miezi nane bila mshahara wangu kurejea. Baada ya miezi hiyo, mshahara ulianza tena kama kawaida. Nilielekezwa kuandika barua ya kudai mishahara ya miezi hiyo nane. Baada ya kuandika barua na kujaza fomu maalumu ya kudai malimbikizo (arrears), kila ninapokwenda kwa HR kuulizia, wanadai kazi yao ilishakamilika na malipo yapo mikononi mwa Hazina.
Nashindwa kuelewa hatua nyingine za kuchukua kwani mtu pekee ninaweza kumuulizia ni DHRO.
Nifanye nini? Na ni mbinu gani naweza kutumia, kwani pia kuna mishahara ya miezi ya mwanzo wa ajira yangu ambayo sijawahi kulipwa hadi leo.
Naomba msaada wenu. 🙏
Sasa mkuu si ungeweza kushauri nini kingefanyika kwa kadhia hiyo aliyoielezea? Hapa kuna wengi utawasaidia!Kwanza ww una bahati utakuwa umekutana na Afisa Utumishi Muungwana,kosa ulilolifanya ni la kufukuzwa kazi moja kwa moja.
By the way Mwambie HR wako mawasiliano ya approver wenu aliyoko Utumishi,huyo ndio anayepitisha kila kitu chenu cha kiutumishi atakuwa anajua shida ni nini.
Siku nyingine usirudie ujinga uliofunya utapoteza kazi ukiwa unaangalia.