KIUNGOMCHEZESHAJI
Senior Member
- Oct 4, 2013
- 120
- 255
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Ninafuga kuku wa kienyeji hapa shambani kwangu. Kwa kweli kuku wanastawi vizuri na nilishaanza kufurahia matunda ya jasho langu, lakini ghafla nilianza kuona mayai yakipungua wakati kuku wanataga kila siku. Niliamini pasipo na shaka itakuwa nyoka. Hivi majuzi tukafanikiwa kumdaka nyoka mkubwa akiwa amemvamia kuku anayelalia. Kuku alianza kupiga kelele usiku ndipo tulipokurupuka na kwenda kuangalia, tukamkuta ameshameza mayai mawili tayari. Tulifanikiwa kumwua huyo nyoka.
Lakini hata baada ya kumwua huyo nyoka, bado mayai yameendelea kupungua. Pamoja na jitihada za kumwaga mafuta ya taa mlangoni na maeneo yanayozunguka nyumba lakini ufanisi ni mdogo. Hii mbinu ya kumvizia nayo ni ya kubahatisha. Je naweza kutumia mtego gani kuwamaliza nyoka shambani mwangu? Au nitumie dawa gani?