Msaada: Nyoka wananimalizia mayai ya kuku wangu

Sio jamii zote za Nyoka wanakula mayai.

Kuna jamii maalum ambao hawali kitu kingine ni mayai tu, na wakishajua chimbo wanaweka kambi...Mleta mada anaweza kuwa sahihi ni Nyoka, ila pia inawezekana yanaibiwa na Mtu.
 
Hapo mdau ni kuimarisha banda, kufanya fumigation kwa sababu ni shambani huwezi kujua makazi yapo wapi....
Ila pia wapo wanaoamini chumvi hudhuru tumbo la nyoka...labda jaribu kumwaga chumvi kuzunguka banda...ni mtizamo tu...POLE na kila la heri....



Everyday is Saturday........... 😎
 
Kuna wadudu fulani ni wakubwa mara mbili au tatu ya sisimizi wakubwa, hao wadudu ni wa kupandikiza kazi yao ni kubugudhi nyoka, nenda kwa watu wa mime au maliasili wata kuelekeza vyema jinsi ya kuwapata.
Pia kuna ukoka fulani majani yake ni mapana yale huwakata nyoka na kuwa bugudhi.
 
Mkuu mi nashangaa maneno meeengi, we chukua chumvi hata ya buku mbili na mwaga kwa wingi eneo unaloona kuna njia ya nyoka, akifika tu nyoka anayeyuka au anakufa na hivyo hakuna nyoka yoyote atakaefika hapo. Nyoka na chumvi hawapatani kabisaa maana anayeyuka au kufa fasta.
Ukiona umeweka chumvi na bado mayai yanaibiwa basi hapo sio nyoka ni binadamu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao wadudu wanaitwa sangara, penye sangara nyoka hasogei...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeambiwa ni sumu ya panya sio sumu ya nyoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu fafanua kwa mechanism ipi nyoka huyayuka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo sumu ya panya si inatoka kwa nyoka! Na mimi nawaza..
 
Nyoka akila yai lazima alivunje ateme maganda sasa yai lililochemshwa akilila hawezi kuvunja kulivunja likishaenda tumboni sisi ndio tulivyokua tunawamaliza kenge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo sumu ya panya si inatoka kwa nyoka! Na mimi nawaza..
Is it? Sina hakika inakotoka maana mmmh sumu ya panya ni kiboko. Kuna mbwa mmoja mmiliki wake alitaka kumuua maana aligeuka tishio mpaka kwa familia. Hivyo anachukua tonge la ugali akaweka sumu panya akampa mbwa. Eeeee Bwana Eeee baada ya muda mfupi mba akawa anatoa udenda tu na taratibu akafa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…