Msaada: Nyumba ya contemporary inavuja

Nilikuwa nazipenda sana nyumba za aina hii hadi nilipojionea kwa ndugu yangu.

Nyumba imeezekwa lakini inavunja sana Pembeni mwa mabati.

Afanyeje ili isivuje?

N.B: Pembeni ukuta umechimbwa ili kuingiza bati na kuzibwa kwa cement ya water proof.

Kuna mbinu ndogo ndogo zinatumika mafundi wengi hawajui! Yangu ilikuwa inavuja pia kifuata ukuta!! Kuna fundi nilimpata mitandaoni nikamuita akaja akapiga cement ya waterproof na kuna gundi maalum inatumika!!

Pia kwa kitumia mbinu za kiufundi alinyanyua paa upande mmoja ili maji yafuate njia!!

Toka hapo kuvuja kwangu nakusikia kwenye mitandao kama hivi!!

Huko pe.beni tafuta fundi wapige cement ya water proof
 
Nikajua hiki kilio ni changu tuu.
nimeshahangaika na uamuzi ulifikiwa ni kubadili designing.
napaua kawaida.
nimekaa mwaka 1 nanyeshewa ndani kama nipo nje.
ukileta fundi ndo anaongeza majanga.
Inavuja gutter..pembeni..katikati ya Bati (kwenye misumari) marekebisho yashagharimu 700 na sasa bora niongeze ml 3 nibadili tuu.
nimechoka aisee
 
Bora hii inanitia moyo.
 
Pole ndugu.
 
Changamoto ya Hizi nyumba ni kuvuja sana.

Binafsi zizipendelei sana.

NYUMBA NI BATI.
 
Nilikuwa nazipenda sana nyumba za aina hii hadi nilipojionea kwa ndugu yangu.

Nyumba imeezekwa lakini inavunja sana Pembeni mwa mabati.

Afanyeje ili isivuje?

N.B: Pembeni ukuta umechimbwa ili kuingiza bati na kuzibwa kwa cement ya water proof.
contermplary kwa nyumba za kuishi za kibongo bongo hazifai, wenzetu huwa wanaweka corridor kuzunguka nyumba na kutengenza water drainage nzuri sana, huku kwety water drainage inaweza kula 30% ya bajeti ya ujenzi wako, usipofanya hivyo lazima ivujishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…