Msaada: Ofisi za wanaoshughulika na ajira portal zipo sehemu gani kwa Dar es Salaam?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Nimekuwa na tatizo kidogo kuhusiana na mfumo wa ajira portal ie online application. Hapo wameweka namba za msaada kama ukihitaji kuwapigia. Lakini hizi namba huwa aidha hazipatikani kabisa au unaambiwa ziko busy!

Sasa nimeamua kufuatilia ofisini na ndio maana naomba maelekezo kwa anayefahamu mahali ofisi zao zilipo ili nikapate msaada hapo.
 
Walikuwa pale Maktaba,nadhani walihamia Dodoma.
 
Wapo dodoma ukiwa sabasaba pale panda gari zinazoenda social halafu shuka utumishi.shida yako itatatuliwa
 
Nimekuwa na tatizo kidogo kuhusiana na mfumo wa ajira portal ie online application. Hapo wameweka namba za msaada kama ukihitaji kuwapigia. Lakini hizi namba huwa aidha hazipatikani kabisa au unaambiwa ziko busy!

Sasa nimeamua kufuatilia ofisini na ndio maana naomba maelekezo kwa anayefahamu mahali ofisi zao zilipo ili nikapate msaada hapo.
Kwa Dar es Salaam Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ipo Posta jengo la UTUMISHI 'Kivukoni Road'

Ni karibu na

1. Stendi kuu ya mabasi ya Mwendokasi Kivukoni

2. Ofisi za TPA na TASAC 'mnara'

3. Wizara ya Ardhi na Makazi

Kwa Dodoma 'HQ', ofisi zipo UDOM - Utawala 'jengo la Utumishi' ~ Asha Rose Migiro Road

Ni karibu na

1. College of Bussiness Studies and Law (CBSL)

2. Karibu na UDOM Social Hall
 
Nimekuwa na tatizo kidogo kuhusiana na mfumo wa ajira portal ie online application. Hapo wameweka namba za msaada kama ukihitaji kuwapigia. Lakini hizi namba huwa aidha hazipatikani kabisa au unaambiwa ziko busy!

Sasa nimeamua kufuatilia ofisini na ndio maana naomba maelekezo kwa anayefahamu mahali ofisi zao zilipo ili nikapate msaada hapo.
mkuu umepata any solution ?
 
mkuu umepata any solution ?
Nimepata solution na nashukuru sana. Nilienda pale jengo la utumishi Dar kwa kufuiata maelekezo ya kina ya Synonym. Hili jukwaa kwa kweli lina utajiri sana wa ukarimu na kujaliana! Nilipofika pale nilihudumiwa vizuri kabisa!!
 
Back
Top Bottom