Msaada: Pilipili na vidonda mdomoni

Msaada: Pilipili na vidonda mdomoni

funduku

Senior Member
Joined
May 2, 2013
Posts
131
Reaction score
36
Habari wana jf doctor.
Bila kupoteza muda Ningependa kwenda moja Kwa moja kueleza juu ya tatizo linalonisumbua kwa muda mrefu sasa

Nina tatizo la kutokwa na vidonda vya mdomo na katika ulimi wakati mwengine hutokea hata kwenye fizi pia.

Hapo mwanzo nilikua bado sijajua chanzo cha tatizo ni nini, lakini baada ya kujichunguza sana hatimae nikagundua kua pilipili ndio chanzo cha tatizo linalofanya nitokwe na hivi vidonda kwani ninapotumia pilipili au chakula chenye pilipili siku ya pili yake au ya tatu vidonda huwanza kutoka mdomoni na siku zinavyozid kwenda vidonda hua vinaongezeka na maumivu huzidi kua makali mno na huchukua wiki moja mpaka mbili kupona kabisa nisipotumia dawa.

Kwahiyo nikagundua kua nina aleji na pilipili kwani hata nikila chakula chenye hata kiasi kidogo sana cha pilpili tatizo huanza

Kwahiyo Naomba ushauri nini cha kufanya ili Nikila pilipili isiwe inanisababishia haya madhara? Maana kila nikijaribu kuacha kutumia pilipili hua nashindwa kabisa. Na vidonda ndio Leo tu vimeanza kupona.

Asanten wakuu, pia samahani kwa maelezo marefu.
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom