Jamani naomba ushauri wenu. Kutokana na mvua za jana ukuta wa nyumba yangu umeangukia kupande wa jirani na kuharibu tenki la maji. sasa nasikia ameenda kushitaki serikali za mitaa.
Je kesi kama hii inakuwaje?
Hakukuwa na sababu ya kesi kama wewe ungeonesha ushirikiano. Kibinadamu ulitakiwa asubuhi uende kwa huyo jirani kwanza umpe pole na halafu mzungumzie huo uharibifu uliofanyika. Hatahivyo utaitwa hapo serikalini na kuambiwa ulipe tu, jiandae.