Kugawana mali sawa kwa sawa bado ni legal issue kwa Tanzania. Kifungu cha 114 kifungu kidogo cha (1) cha sheria ya ndoa (Marriage Act, 1971) Kinasema "The court shall have power, when
granting or subsequent to the grant of a decree
of separation or divorce, to order the division
between the parties of any assets acquired by
them during the marriage by their joint efforts
or to order the sale of any such asset and the
division between the parties of the proceeds
of sale."
Legal issue hapo ni nini iwe tafsiri ya "joint efforts" Hapa tunapata dhana za mawazo aina mbili, yaani, broad sense na narrow sense. Narrow sense hudhani kuwa 'joint effort' ni jitihada za kifedha, mali na kazi, huku 'broad sense wakidhani 'joint efforts' ni msaada wowote ambao mume au mke ameutoa katika familia. Lakini Tanzania tunashikilia msimamo wa narrow sense kama ulivyotumiwa kuamua shauri la madai ya mali za ndoa katika kesi ya (Mohamed v Sefu (9 of 1983) [1983] TZCA 1 (29 November 1983) ambapo Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilishikilia msimamo kuwa ili mali za ndoa zigawanwe pasu kwa pasu sharti kuwepo na mchango wa kifedha, mali au kazi tofauti na kazi ya kulea watoto na kazi za nyumbani kutoka kwa mdai wa mgawanyo huo. Hivyo ni vigumu kwa mwanamke kugawiwa mali pasu kwa pasu ya ndoa isipokuwa akionesha kwa ushahidi usio na shaka kuwa alitoa mchango wa kifedha, mali au kazi.