je? kuna sheria yoyote inayo mfunga mtu aliyeishi na mwanamke takribani 2 bila kuwa na legal document kama wameoana. na endapo mwanaume akiamua kumuacha kuna sheria yoyote inayomulinda mwanamke kudai fidia, na fidia itakuwa kiasi gani.
kuna ndugu anahitaji msaada wa mawazo yamemkuta.
ndio, inapotokea kua mwanamke na mwanaume wameishi kama mke na mume kwa miaka miwili au zaidi, kuna sheria inayomlinda mwanamke katika Marriage Act.je? kuna sheria yoyote inayo mfunga mtu aliyeishi na mwanamke takribani 2 bila kuwa na legal document kama wameoana. na endapo mwanaume akiamua kumuacha kuna sheria yoyote inayomulinda mwanamke kudai fidia, na fidia itakuwa kiasi gani.
kuna ndugu anahitaji msaada wa mawazo yamemkuta.
ndio, inapotokea kua mwanamke na mwanaume wameishi kama mke na mume kwa miaka miwili au zaidi, kuna sheria inayomlinda mwanamke katika Marriage Act.
Ili mwanamke huyo apate haki yake, inapaswa kutoa ushahidi kuwa waliishi na mwanaume kwa miaka miwili au zaidi, waliishi kama mume na mke na pia hata watu waliowazunguka walifahamu juu ya mahusiano yao.
Endapo kuna mali ambazo walizipata wakiwa wanaishi pamoja, katika kuachana, mali hiyo itagawiwa sawa kwa sawa.
Kugawana mali sawa kwa sawa bado ni legal issue kwa Tanzania. Kifungu cha 114 kifungu kidogo cha (1) cha sheria ya ndoa (Marriage Act, 1971) Kinasema "The court shall have power, when
granting or subsequent to the grant of a decree
of separation or divorce, to order the division
between the parties of any assets acquired by
them during the marriage by their joint efforts
or to order the sale of any such asset and the
division between the parties of the proceeds
of sale."
Legal issue hapo ni nini iwe tafsiri ya "joint efforts" Hapa tunapata dhana za mawazo aina mbili, yaani, broad sense na narrow sense. Narrow sense hudhani kuwa 'joint effort' ni jitihada za kifedha, mali na kazi, huku 'broad sense wakidhani 'joint efforts' ni msaada wowote ambao mume au mke ameutoa katika familia. Lakini Tanzania tunashikilia msimamo wa narrow sense kama ulivyotumiwa kuamua shauri la madai ya mali za ndoa katika kesi ya (Mohamed v Sefu (9 of 1983) [1983] TZCA 1 (29 November 1983) ambapo Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilishikilia msimamo kuwa ili mali za ndoa zigawanwe pasu kwa pasu sharti kuwepo na mchango wa kifedha, mali au kazi tofauti na kazi ya kulea watoto na kazi za nyumbani kutoka kwa mdai wa mgawanyo huo. Hivyo ni vigumu kwa mwanamke kugawiwa mali pasu kwa pasu ya ndoa isipokuwa akionesha kwa ushahidi usio na shaka kuwa alitoa mchango wa kifedha, mali au kazi.
Sheria ya ndoa ya tanzania inazungumzia dhana ya ndoa(pressumption of marriage) ni pale m'me na m'ke wanapoishi pamoja kama mume na mke na jamii ikawapa hadhi ya wanandoa kwa muda wa miaka 2 na zaidi na c miez sita kama ulvojibiwa.
Kwakuwa hii ni dhana tu hvyo yaweza kukanushwa na mmoja wenu,na iwapo itathibitika mdai talaka atakua entittled rights zote kama za ndoa halisi.Hivyo bas mdai huyo atafuata taratib zote za ufunguaj wa shauri la madai ya talaka ambapo ataanzia baraza la usulihish wa mambo ya ndoa ofis za kata au ustaw wa jamii ambako kna form atapewa huko na kuipeleka mahakaman kufungua shaur hlo.huko ndio namambo ya mgawanyo wa mali mlzochuma pamoja yataamuliwa.
Umeongea vizuri sana ndugu, . bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILIkwanza pole sana kwa yote yale unayopitia. Pili ni kuwashukuru wale wote ambao wameweza kuchangia katika thread hii.Lakini nitaomba nitafautiane na baadhi ya wachangiaji wa awali ambao wametoa yale waliyosema.Pia naomba nieleze tuu kwa lugha raisi bila ya kufanya nukuu za vifungu vya sheria au maamuzi ya kesi mbalimbali. Pengine nitoe pia tahadhari kwamba dhana ya ndoa kama ilivyoelezwa na baadhi ya wachangiaji iko kidogo technical. Kujibu swali ni kwamba mke anayeishi katika dhana ya ndoa anapata stahili nyingine kama ilivyo mwanamke anayeishi katika ndoa ila hawezi kuomba divorce au separation, na huyu mama anakuwa considered as deemed legal wife. Ila linapokuja swala la kugawana mali walizochuma hawezi kutumia hicho kifungu cha 114 kwani hicho ni kwa wale walio na ndoa ambazo zilifuata zile taratibu zote za ndoa, kumbuka huyu mama hana ndoa but just a presumption of marriage . Hivyo huyo mama hatadai hizo mali kama mke wa huyo jamaa ila kama mtu mwingine au just a business partner. Hivyo huwezi kusema ni kugawana nusu kwa nusu litatagemea ushahidi uliopo. Ila kuna njia ambayo ni technical chini ya hiyo sheria ya kuweza kumsaidia huyo dada/mama. Ila sitasema hapa ili kuwezesha advocates kula hela za dezo, na hata akihitaji precedent ipo tuu tena bila shaka yoyote. aksanteni n gdy
je? kuna sheria yoyote inayo mfunga mtu aliyeishi na mwanamke takribani 2 bila kuwa na legal document kama wameoana. na endapo mwanaume akiamua kumuacha kuna sheria yoyote inayomulinda mwanamke kudai fidia, na fidia itakuwa kiasi gani.
kuna ndugu anahitaji msaada wa mawazo yamemkuta.