Lady G, pole kwa usumbufu unaoupata,
Kwenda haja ndogo mara kwa mara si dalili ya mimba, ingawa mimba ikiwa kubwa utakuwa unakwenda haja ndogo mara nyingi kwa sababu uterus inapokuwa huwa inakandamiza kibofu cha mkojo na hivyo kupunguza capacity yake, so mkojo kidogo kibofu kinajaa kwa sababu kimekuwa kidogo na hivyo utakwenda chooni mara kwa mara, lakini sio dalili ya kwanza ya mimba.
Sijui umekutana lini na Mr wako lakini a week after conception kile kipimo cha mkojo (UPT) huwa kinakuwa positive. Hivyo kama una wasi wasi check kwa UPT.
Dalili za mwanzo za mimba ni kichefuchefu ambacho huambatana na kutapika hasa nyakati za asubuhi (Morning sickness), pia utakosa hamu ya kula au utakuwa unachagua sana aina ya vyakula, mbali ya hapo ile sehemu nyeusi inayozunguka chuchu (areola) itakuwa nyeusi zaidi kuliko kawaida, utapata mstari mweusi katikati ya tumbo chini ya kitovu (linea nigra), hizi ni chache ya dalili nyingine.
Natumaini umenielewa, utakuwa na mimba kama tu hizi dalili unazo na kucomfirm ni lazima ufanye hicho kipimo cha UPT au Obstetric Ultrasound (vaginal ultrasound).
Kwenda chooni mara nyingi huwa ni dalili ya uambukizo kwenye njia ya mkojo (Urinary Tract Infection) na hasa kama inaambatana na maumivu wakati wa kukojoa (dysuria).
Njia ya uzazi wa mpango uliyoitumia (coitus interruptus), sio njia nzuri sana ya kupanga uzazi, most of the time inafeli, ni lazima mwenzi wako awe very much commited na wakati mwingine huwa ngumu hata kwa mtu ambaye yuko commited, si unajua utamu wa orgasm ni ejaculation within the vagina.