Msaada pls

Usiku anaamka ananiambia dada mbona mimi nimetulia, au mimi ni mbaya, mbona nina tabia nzuri, sijawahi kumsaliti, sijawahi kulala na mtu zaidi yake yaani, nyumba imekuwa kama msiba hakujawashwa redio wala TV

i real feel sorry for her!!!

Namuombea Mungu tu, sina cha kumwambia!!!!
 
Naomba nijue ukweli.. wewe kama dada yake lazima umemsoma.. vipi yeye binafsi anataka kuamua vipi?? Na the guy vipi siku zoote mpaka sasa vipi attitude yake??

Kwa jinsi nilivyomsoma na maongezi yake hataki kuwa na jamaa tena, anasema jmaa sasa hv attention iko kwa mtoto wake sana kwa hiyo hawezi kumjali yeye jamaa alikuwa mtu mzuri sana mapenzi ya dhati, ila huwezi kujua moyo wa mtu labda alikuwa anapretend sijui
 
Ajipe muda wa kufikiri kama one week au zaidi, then atakuja na uamuzi mzuri, kwa sasa hawezi kufanya uamuzi sahihi kwa sababu ni jana tu amegundua hilo. mapenzi ya miaka nane siyo mchezo, hayawezi kuamuliwa just in one day.
 

Sometimes, I______________________men, argh!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Joyceline:
It seems like huyo jamaa doesnt care for your sister as much as you and/or your sisters think he did/does. It's ok , and noble for him to want to take
care of his child but that doesnt justify
1. Yeye kumficha mdogo wako habari za mtoto from beginning
2. Yeye kumnyang'anya hilo gari kama alishampa toka mwanzo
Unless she is ready to be the second best to the baby mama, aachane nae!
 
huyo jamaa alizaa kwa bahati mbaya, shetani alipita, ila kwa ustaarabu wake hakutaka kumshawishi msichana kutoa mimba, na alipozaa hakumtelekeza. Muda wa kumweleza mchumba wake anaujua mwenyewe kwani anamfahamu vizuri, timing inatakiwa au utavuruga zaidi. Kama mda wote walikaa vizuri hili si kosa la kuvunja uchumba. Wamwombe mungu awaimarishe wasianguke tena katika vishawishi
 
Usiku anaamka ananiambia dada mbona mimi nimetulia, au mimi ni mbaya, mbona nina tabia nzuri, sijawahi kumsaliti, sijawahi kulala na mtu zaidi yake yaani, nyumba imekuwa kama msiba hakujawashwa redio wala TV

Mhhhh! Maneno mazito sana haya tena yanaumiza kweli. Kama alivyoshauri TF mdogo wako kwa sasa hastahili kuachwa pekee yake anaweza kuchukua uamuzi ambao si mzuri kwa kweli. Hakikisha kunakuwa na mtu anamuangalia mpaka pale atakapoonekana ana ahueni japo kidogo.
 


Ni afadhali kama ana msimao huo... I really don't know what to say...
 

Mmmh, hapo ndo kwenye utata. Jamaa kaamua kwenda nje sababu mdogo wako hazai. Mdogo wako awe makini naye sana maana kwa jinsi ninavyoelewa ndoa ni zaidi ya mtoto. Japo unasema kafanyiwa operation, jee mimba isiposhika? Na mbaya kampangishia hapa Dar, achanganye vizuri akili.
 

Mhhhh! inauma sana!
 
She needs counselling first, and she doesnt have to rush into any decision now,she shouldn't make a decision which she is going to regret for the rest of her life, what she decides today will determine what the future will hold for her tomorrow, not all married people are living happily in their marriage life
 
Ndugu yangu hii situation ni ngumu sana sana ishu ni kwamba hawa wapenzi wawili kuna maongezi wanayoongea wakiwa wawili ambayo wewe huyo mdogo wako anakuficha. Kumbuka jamaa anaongea nae wakati ana muuma sikio au wapo kitandani!!!! kwa mahaba na maraha na inawezekana labda mdogo wako hajawahi fanyiwa hayo mambo. So inakuwa ngumu kumwambia ukweli mkiwa sebuleni nyie na nduguzo!! kavu kavu tu na kumsimanga ??umeona utata! Solution ni kwamba wakutanishe wote wawili na huyo mwingine aliye zalishwa waongee wao wajue mustakabali wao.. na mwisho wakutanisheni wote wa tatu kwani nina hakika kwamba jamaa ana kataa kwamba hana mtoto na hana mausiano na mtu yeyote. Ni hayo tu ila mdogo wako anakifua? asije kufa bureeeee.
 

Naona jamaa bada ya kupiga hesabu za miaka minane na mimba mbili ambazo hazikuwa na mafanikio kaamua kuingia mitini, labda huyu wa Arusha haikumchukua muda mrefu kushika mimba na hatimaye kupata mtoto wake wa kwanza. Poleni sana, nasema poleni maana na wewe hili linakuathiri kwa namna moja au nyingine. Ukimuona mdogo wako anaumia na wewe lazima utakuwa unasononeka.
 
YouTube - Aaliyah - The One I Gave My Heart To (Music Video)
 
Inauma sana aisee......i understand jinsi mdogo mtu hali aliyonayo sasa hivi it's difficult but life has to go on
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…