jamani tukisemea experience za maudhi ya mimba hapa tutashangaa wenyewe. huwa napenda sana kutumia experience yangu mwenyewe.
nikiwa mjamzito wa 1st born wangu, ilipofika wiki 38 nilianza kuumwa sikio la kushoto, sijawah kuliingiza maji, wala kitu chochote hata iwe pamba lkn liliuma kama nakufa hivi. kwenda muhimbili, wakasema wananilaza, nilifanyiwa x-ray kuangalia kuna nn hakukuwa na fungus wala bakteria na mbaya zaid linawaka moto sana na linatoa maji maji yalipopimwa na kuwa cultured pia hakukuonekana bacteria ambao ni threat. unajua nn siku moja dr anjela thomas alisema hebu leo tumpime njia lolest, sina uchungu wala nn lkn njia ilikuwa imesha funguka cm 5, chupa haijavunjika wala sina dalili yyte ya labour zaid ya sikio tu. you cant believe ilibidi waniwekee maji ya uchungu ili nizae tu na ukweli uchungu ulipoanza tumboni sikio lilikoma na mtoto akazaliwa.
anyways nia yangu hapa nataka nikuonyeshe ndugu mtoa mada kwamba, maudhi ya mimba ni mengi na hayana clinical explanation ila kama kapimwa hana shida yyte ile basi usimsumbue kung'oa vumilie tu huku akitumia pain killer. pole yake sana tu.