Wadau naombeni kujua ni process gan nifuate ili nipate leseni ya biashara
Mkuu Naivasha niliongelea kuwa tanzanialifeclub.com wanasaidia hii issue ulikuwa wa kwanza kuponda vipi ungewasiliana nasi ukapata huduma hii na ushauri haraka iwezekanavyo.Jamani wana JF nami ninahitaji msaada wa kupata leseni. Nimesajili kampuni, nimepata TIN sasa nahitaji Business License zinazotolewa na wizara ya Viwanda. Naomba maelekezo ya namna au taratibu za kufuata. asanteni
Mkuu Naivasha niliongelea kuwa tanzanialifeclub.com wanasaidia hii issue ulikuwa wa kwanza kuponda vipi ungewasiliana nasi ukapata huduma hii na ushauri haraka iwezekanavyo.
Wadau naombeni kujua ni process gan nifuate ili nipate leseni ya biashara
leseni ya biashara hutelewa bure na halimashauri ya eneo husika, sina hakika kwa habari za wilaya, lakini nadhani wanawajibika kwenda mkoani kupata lesseni hizo. hutolewa na afisa biashara.
taratibu zake,
1. unapaswa kwenda kwa afisa biashara aliyekaribu na wewe
2. utapewa fomu pamoja na kulipia, tsh. 1,000/- tu
3. fomu hizo utapewa na kuzijaza kuanzia ngazi ya mtaa, kata ndipo kwa afisa biashara wa eneo lako.
4. ukishatoka hapo, utawajibika kwenda TRA, ambapo wataandaa file lako na kuchukua picha, alama za vidole, na kutathimi kodi unayopaswa kulipia kwa mwaka.
5. TRA watakupa TIN namba, na utatakiwa kulipa kodi yako at least kwa miezi minne ya mwanzo.
6. ukisha pata TIN namba, unarudi kwa afisa biashara anakuandikia lesseni ya biashara.
malipo yanayohusika ni TIN namba pekee kama kodi yako na sh. 1,000/- ya fomu ya maombi ya lesseni ya biashara. kama utadaiwa pesa zaidi ya hiyo, jua hiyo ni rushwa na huyo si mtumishi wa haki, bali ni mtumishi mwovu. unaweza ukaamua kumchukulia hatua stahiki.
hutolewa bure kabisaa. na wengi tunaingia kwenye skendo ya kutoa hela kwa kuwa hatujui, na wengi tunafanya biashara bila kuzisjaili kitu ambacho ni hatari kwa biashara yako siku ukibainika na ni hatari kwa wateja wako kwani wanawezwa kufunguliwa kesi polisi kukutwa na mali ya wizi.
linda biashara yako, ni rahisi mno
angesaidiwa na lifeclub asingejifunza hizi hatua.
mie mwenyewe nimeshaandaa memorundum na articles of association naenda brela mwezi May.
Naapa siwez kuja lifeclub kwa kuwa ntapoteza fursa ya kujifunza ugumu na urahisi wa hatua za usajili n.k
mkluu hata mm nimeipata hiyo...goodPaxman nimekupata. Tunahitaji kujifunza au kwa maana nyingine tunahitaji kutembea kwa miguu yetu. Sasa mtu unaomba msaada wa maelekezo tu pembeni anadakia mtu hatoi maelekezo bali anadai eti atakufanyia. Huu ni udalali ambao unamuongezea mtz ukali wa gharama za maisha. hoja inaanza vizuri vishoka wanaharibu sio nzuri. Mi nawashukuru wote waliotoa maelekezo ya namna mtu anavyoweza kupata leseni n.k. Mimi yawezekana nina matatizo kwani huwa sipendi kufanya kazi na hawa jamaa middlemen. Asanteni sana