Msaada: "Rice Cooker vs Slow Cooker" ni kitu Kimoja?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu mambo vipi?

Nina likizo ya week 3 kazini. Nitakua ghetto muda wote huo. Sa nitakua napika pika maana kununua gharama sana.

Sasa nimekutana na kitu kinaitwa Slow Cooker, je ndio hiyo hiyo Rice Cooker au vitu tofauti?

Kwa kifupi nataka dude litakaloweza kupika nyama, wali, mbogamboga etc. Yaani all in 1.

Shukrani.
 
Zipo tofauti, slow cooker inatumia joto dogo na kuivisha chakula kwa muda mrefu zaidi....rice cooker inatoa joto jingi zaidi na kuivisha chakula kwa muda mfupi.

Slow cooker ingekufaa zaidi kama unataka kupikia vitu mbali mbali ila kama ungekuwa na muda na unataka kufurahia chakula bora utumie jiko la kawaida uwe na sufuria zako na frying pan!
 
Unatakiwa uwe nazo zote tatu, slow cooker unapikia chakula kigumu kinakuwa laini na test tamu kama vile umepikia chungu hii ni vizuri kuweka chakula usiku ukiamuka unakuta chakula tayari maana nyingi zinajizima, vyakula vya kupikia slow cooker nyama ya ng'ombe na Asubuhi unaweza kutumia supu kwa breakfast, kuku wa kienyeji hivyo hivyo, Rice cooker utapikia wali na tambi na kama inakifaa cha steam utachemshia mayai na vegetables.

Pressure cooker hii vyakula vyote ila siyo vizuri kuipikia wali hautoki vizuri kingine chakula cha kupika kwa pressure cooker kinaiva haraka kama maharage na umeme kidogo na vingine kama nyama dakika 10 imeshaiva, ndizi, viazi, mihogo, karanga za kuchemsha dakika 10 au 5 tayari chakula kimeiva hivyo ni muhimu kuwa nazo zote tatu.
 
Kanunue MULTI PURPOSE PRESSURE COOKER AINA YA "ELSHERIF" NI DUDE LA UHAKIKA. UNAPIKA UNA OKA,UNA CHEMSHA,UNA PASHA,UNA KAANGA NA LINA TUMIA UMEME KIDOGO MNOOO! MAPISHI NI SEKUNDE TU NYAMA NI DK 10 TU UMEKULA KITU LAINIIIII !!!
 
Ukiunga tunapata Rice slow cooker
 
Duh pressure cooker ,tunapoelekea tutaletewa magnetic cooker,induction cooker ,volume cooker nk
 
Kanunue MULTI PURPOSE PRESSURE COOKER AINA YA "ELSHERIF" NI DUDE LA UHAKIKA. UNAPIKA UNA OKA,UNA CHEMSHA,UNA PASHA,UNA KAANGA NA LINA TUMIA UMEME KIDOGO MNOOO! MAPISHI NI SEKUNDE TU NYAMA NI DK 10 TU UMEKULA KITU LAINIIIII !!!
Mkuu naomba kujua wastani wa being kwa hio
 
Zipo tofauti, slow cooker inatumia joto dogo na kuivisha chakula kwa muda mrefu zaidi....rice cooker inatoa joto jingi zaidi na kuivisha chakula kwa muda mfupi.

Slow cooker ingekufaa zaidi kama unataka kupikia vitu mbali mbali ila kama ungekuwa na muda na unataka kufurahia chakula bora utumie jiko la kawaida uwe na sufuria zako na frying pan!
Masaki mnaita frying pan ila kwetu huku tunaziita flampeni 😂🤣
 
Kanunue MULTI PURPOSE PRESSURE COOKER AINA YA "ELSHERIF" NI DUDE LA UHAKIKA. UNAPIKA UNA OKA,UNA CHEMSHA,UNA PASHA,UNA KAANGA NA LINA TUMIA UMEME KIDOGO MNOOO! MAPISHI NI SEKUNDE TU NYAMA NI DK 10 TU UMEKULA KITU LAINIIIII !!!
Inauzwaje hiyo MULTI PURPOSE PRESSURE COOKER, na kwa ujazo upi,?asante
 
Back
Top Bottom