Msaada: Rim/Tyre size na Tyre Pressure kwa Toyota Premio

Msaada: Rim/Tyre size na Tyre Pressure kwa Toyota Premio

Msolid1990

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
144
Reaction score
50
Wakuu,
Nina Toyota Premio f niliagiza kutoka Japan mwaka jana mwishoni. Gari imekuja na rim size 14 na nikipita barabara ya vumbi kuna wakati inagonga sana chini, kwenye mlango wa dereva kwa pembeni kuna hizi options zimeandikwa kama inavyoonekana kwenye picha niliyoambatanisha hapa(Pamoja na tafsiri yake kwenye Kiingereza kwa kutumia google lens)
Hapo kwenye picha upande wa tyre size naona kuna options 2
  1. 185/70R14 88S na
  2. 195/65R15 91S
Nafikiri kwa kuangalia rim size hii gari imekuja na hiyo option ya kwanza, Je nikiweka hiyo option ya 2(Rim 15) gari itapanda juu kidogo? maana naona kuna hiyo number hapo badala ya kuwa 70 inakuwa 65 ndo nawaza isije kuwa haitabadilisha chochote.

Issue ya pili ni Huo upande wa Tyre pressure naona hapo front wheel imeandikwa 230 na na rear wheel 200, je kwa wataalamu hii ina maana gani? Maana nilienda kucheck upepo kwenye kituo Fulani cha mafuta wakaniambia mbele inatakiwa 30 na nyuma 35 ndo wakaweka hiyo. Hii imekaaje isije ikawa naweka upepo ambao sio sahihi kulingana na maelezo.

Asanteni sana.

img1.jpeg
Img2.jpeg
 
Nakushauri weka rims za size 16 nadhani ndiyo maximum size kwa Premio or Allion.
Mimi mwenyewe nilikutana na same scenario

Niliagiza Allion ilikuwa na size 14 nikaweka Spacer baadae nikaja kuweka rims 16 na tyre 165/55 ikapanda juuu,
Sikwami popote.

Kwenye mlango nadhani wameandika maximum size 16 kwenye Allion, ambayo nahisi haitofatiani na Premio.
 
Mkuu naomba kuuliza mpaka inakufikia mkononi ulitumia kiasi gani hii premio F?
Mkuu hii nilitumia 17M bila bima na vitu vingine baada ya kuipokea. Ukichangana na hivyo vitu vingine ilienda hadi 18M japo inategemea maana mimi bima nilikata comprehensive.
Gharama za gari kutoka Japani hadi kufika bandari ya Dar(CIF) ilikuwa $4,000 kwa kipindi kile dola ilikuwa haijapanda sana so ilikuwa kama 9,400,000 hivi Japo documents zilitumwa na bei ya chini so ikawa nafuu kwenye kodi.
Kwa sasa hivi nafikiri bei zimepanda kutokana na kupanda kwa dola na pia January mwaka huu kodi ilipanda kidogo.
 
Back
Top Bottom