Wasalaam,
Wakuu kwa wale wenye uzoefu wa masuala haya, mwanzoni wa mwaka jana tulifanikiwa kusajili NGO yetu wizarani, na kwa bahati mbaya kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu hatukufanikiwa kufanya shughuli yoyote ya taasisi kwa mwaka mzima ikiwa ni malengo yetu kwa mwaka ujao kuwa active.
Tayari tumepokea ujumbe wa kuwasilisha report ya mwaka mzima ya shughuli za taasisi, ada ya mwaka pamoja report ya ukaguzi, je ni kwa namna naweza kuskip hii au kuwaeleza wahusika juu ya kutokufanya kazi kwa taasisi kwa mwaka unaoisha?
Natanguliza shukrani.
Wasalaam,
Mla Bata.
View attachment 2453558