Msaada: Sheria za kazi za tz kibarua mwisho muda gani?

Paje

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2010
Posts
1,185
Reaction score
486
hello JF
kwa mujibu wa sheria za kazi hapa TZ inabidi kibarua anaweza kufanya kazi kwa muda gani bila ya kuajiriwa na kukatiwa bima (nssf na nk.)

maana nahisi kama napoteza haki zangu
 
Pole Mkuu kwa kudhulumiwa haki zako.

kwa mujibu wa sheria ya kazi kibarua ni ndani ya miezi sita tu!! ukizidisha hata siku mmoja unatakiwa ukarepot kwenye vyombo husika vya kazi na sheria!!

ila fanya hivyo kama una uhakika na kama kuna mkataba uliopewa kimaandishi kuwa wewe ni kibarua halali na una kitambulisho.

Unaweza kupoteza kazi yako bure, sometime ni bora uendelee kuwa kibarua kuliko kufungua kesi. Boss anaweza akahonga halafu wewe ukakosa hata kibarua chako,

Kazi ni kwako mkuu kama upo tayari kujilipua jilupue tu , na ukilianzisha balaaa jua moto utawaka kweli kweli

Halafu mfano umefanikiwa wakakupa shavu hapo ofisini kwa lazima, dah sipati picha ofisi nzima wanakuchukia kwa kuwafungulia mashtaka, hawakawii kukutafutia sababu ufukuzwe kazi. ukichelewa ofisini hata sekunde moja tu unakuta barua ofisini.

Mi nakushauri uongee na wahusika hapo ofisini wakushauri ni jinsi gani utaweza kupata kazi hapo, waeleze kuhusu uzoefu na miezi sita kuwa imefika,ila wasijue kama unataka HAKI.

CHEERS mkuu!!!
 
Acha kumuogopesha,

Tukiwa waoga namna hiyo hatuwezi kupata haki zetu, habari ya watu watakuangaliaje ofisini, ooh mara boss wako atakuchukia sio za msingi, suala ni kwamba una haki ipi na je unaipata na kuifurahia haki hiyo, kama huipati itafute bila kujali "watu" watakuangaliaje! Unaweza ukaenda ofisi yeyote inayotoa msaada wa kisheria wakakupa ushauri zaidi.

Naendelea kukushauri kuwa, usiwe mjinga, pigania haki zako no matter what.

Back
Top Bottom