Msaada: Shule ya A-level inayofundisha PGM kwa wasichana

Chigwiyemisi

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
531
Reaction score
228
Wadau heshima mbele..
Naomba kujuzwa shule nzuri ya wasichana ambayo wanafundisha Combination ya PGM. Binti yangu amefaulu vizuri Form IV na ufaulu wake unamuwezesha kusoma PCM au PGM.

Kwa sasa amepata shule yenye PCM lakini yeye anapenda sana kusoma PGM. Naomba msaada wa ushauri kwani napenda asome course anayopendelea.
 
Kaa nae,umueleze kwa system ya elimu ya TZ,hiyo combination anayotaka itakuja kumbana kwenye machaguo ya kozi chuo kikuu

Na inawezekana target yake ni urubani,pia kaa nae mjadiliane na muangalie kama mnaweza kumudu kumsomesha katika vyuo binafsi,although hata PCM inaweza kumlead kwenye urubani katika mitaala ya nchi za wenzetu
 

Mkuu uko pamoja sana na mimi. Huyu binti ndoto yake ni kuwa rubani. Mimi nilisoma PCM na ni Engineer nilipenda awe kama mimi lakini naona ananikubalia mimi kwa kuniheshimu tu lakini moyoni mwake anapenda kusoma PGM.
 
hata PCM inaweza kumlead kwenye urubani katika mitaala ya nchi za wenzetu

Hapa sijaelewa vizuri, kama hili linawezekana inatakiwa hii PCM akasomee huko au anaweza kuisoma hapa na akapata chuo huko chenye kumwezesha kusomea masomo ya urubani. Nisaidie tafadhali
 
Hapa sijaelewa vizuri, kama hili linawezekana inatakiwa hii PCM akasomee huko au anaweza kuisoma hapa na akapata chuo huko chenye kumwezesha kusomea masomo ya urubani. Nisaidie tafadhali


Hiyo PCM anaweza kuisoma hapa hapa nyumbani na kule akaenda kusomea urubani,kuna vyuo vingi outthere vinavyotambulika hapa kwetu aweza kwenda na kusoma..Kuna vijana wengi wa kiTZ wapo Russia na South Africa ,wengine wamesoma Mzumbe na wanafanya vizuri tu kule
 

Nashukuru mkuu kwa mchango wako.
 
ifunda girls bonge la xkul kwa hyo comb na ifunda technical
 
Usimvunje moyo mtoto,katika hiyo combination ya PGM hapo kuna Physics na Mathenatics hata kama itatokea ukashindwa kumgharamia huo urubani hayo masomo mawili yana very wide selection for high learning courses.Kuna shule inaitwa St.Anne Marie Academy iko Mbezi kwa Msuguli wanafanya vizuri,jaribu kufuatilia.
 
Enzi zangu ljs morogoro sjui kama bado wako vzur bt ni mixture
 
yap kila ktu kpo poa pale tena imeimarishwa dis tym hata ujnga hamna tena
 
mpeleke ifunda girls labda akazngue mwnyw au tech zote zko poa tech washafanya ukarabati
 
Hebu kaa na mwanao umshaur kma mzazi PGM then aje awe nani nchi hii kwa ushaur mwambie apige PCB
 
Hebu kaa na mwanao umshaur kma mzazi PGM then aje awe nani nchi hii kwa ushaur mwambie apige PCB

Are you serious mkuu?

Umewahi kuwaona wangapi waliosoma PGM wakafaulu alafu wamelost?
 

Kuna Ifunda girls ipo Iringa, hii kuna baridi sana huko. Pia kuna Tambaza high school Dar, hapa uhakikishe binti anajitambua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…