Anyway,sio kila kila mara mtu anapotokwa na jasho sana basi ana ugonjwa.Mara nyingi watu wanatokwa na jasho jingi bila ya sababu ya msingi.
Kwenye ngozi yetu kuna vijitezi vidogo vidogo vinavyotoshatoa jasho.Vinafanya hivyo kama njia ya kutoa nje taka mwili.Katika mazingira ya joto kama dar na of course kibaha kuna joto,kwa hiyo si ajabu mtu kutokwa jasho jingi.
Uweza kuuliza,ni kwanini inatokea tu unapokuwa umekunywa maji? Jibu ni kwamba,ktk mazingira ya joto mwili unafanya kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa joto la ndani ya mwili linabaki ktk viwango vyake vya kawaida badala ya kupanda ili kuendana na hali ya hewa.Sasa njia pekee ya kufanya hivyo ni kutoka jasho jingi na kuamsha kiu ya kunywa maji - maji ya baridi.Kwa hiyo basi,unapokuwa umekunywa maji ya baridi,unakuwa umewezesha mwili kufanya kazi yake sawa sawa - kupoza kiu na kwa kufanya hivyo unakuwa ni kama umeusaidia kupamp jasho jingi zaidi.
Chukulia mfano unapokula chakula cha moto..tumbo linakuwa limebeba kitu chenye joto kubwa kuliko joto la mwili,sasa ili kuhakikisha joto la mwili halipandi ili kufuata lile la chakula cha tumboni,basi mtu ataanza kutoka jasho na kusikia kiu.Na ndio maana kiu kinapozwa kwa maji ya baridi.
Swali lingine linawezakuwa,ni kwanini miaka yote hiyo hali hiyo haikuwepo? Jibu ni kwamba binadamu sio jiwe! Kunakuwa na mabadiliko kila siku inayoitwa siku.Watafiti wanasema,kuna wakati vijitezi vya jasho vinakuwa vinafanya kazi zaidi ya kawaida(hyperactive). Haijafahamika ni kwa nini inatokea hivyo,ila habari njema ni kwamba,inatokea hivyo bila ugonjwa wowote mwilini. Na mara nyingi hii hali baada ya muda hupotea yenyewe na hapa pia haijulikani ni kwa nini inapotea tena!