CHAI CHUNGU
JF-Expert Member
- Feb 20, 2012
- 7,113
- 933
Habari wana jf.
Nina mpango wa kulima mahindi na matango kwa ajiri ya kuyauza kwenye soko la ndani,
Napenda kujua kama kuna anayejua soko limekaaje?I mean ntafanya biashara au itakula kwangu?nimepata shamba maeneo ya Iringa vijijini na nimepanga kuuzia shambani,jee mahindi mabichi na matango naweza kuuzia shambani kwa bei gani?nimepanga kulima hk 10 za mahindi na 10 za matango!
Naombeni msaada wakuu.
Poa mkuu malila,ni maeneo ya "IDODI"na nimepanga kumwagilia,Iringa vijijini kubwa, ni kijiji gani? nauliza kwa sababu vijiji vingine wakati wa mvua mafuso hayafiki( ukichelewa kuuza yakiwa mabichi inakula kwako), vijiji vingine mvua za wasiwasi. Vijiji kama Ihimbo/Itimbo msimu uliopita kigunzi kimoja kilifika sh 100 shambani. Na eka moja ikipandwa vizuri inakupa vigunzi 12,000. Na wastani ni vigunzi 8000 kwa eka. Ukiuza pale pale shambani utapata 800,000/ kwa kila eka.
Ila kama unaweza kulima kwa kumwagilia, utapiga hela vizuri. Nenda Mgama pale karibu na Ihemi ukaone kazi za gobo.
Poa mkuu malila,ni maeneo ya "IDODI"na nimepanga kumwagilia,
Jee unafahamu distance ya kupanda mahindi mche-mche?
Poa mkuu,ngoja ni cheki na ma bwana shambani kwanza,Kama utamwagilia, itakuwa bomba sana kwa sababu utayatoa magobo yako wakati ambapo kuna low supply. Nimepita january pale kijiji cha Ukumbi, kuna jamaa ana mahindi yamebeba mawili mpaka matatu na alikuwa anayatoa kupeleka town, ila shamba sio kubwa, nilitamani.
Nakumbuka ni ft moja kt ya mhindi na mhindi kama utapanda moja moja kwa mita moja kt ya msitari na msitari. Lakini hapa inategemea na aina ya mbegu unayotaka kutumia. Mtafute bwana shamba wa maeneo ya Idodi ili akupe data za mbegu.
Lima na alizeti mkuu, Idodi ndio kwenyewe kwa alizeti.
Iringa vijijini kubwa, ni kijiji gani? nauliza kwa sababu vijiji vingine wakati wa mvua mafuso hayafiki( ukichelewa kuuza yakiwa mabichi inakula kwako), vijiji vingine mvua za wasiwasi. Vijiji kama Ihimbo/Itimbo msimu uliopita kigunzi kimoja kilifika sh 100 shambani. Na eka moja ikipandwa vizuri inakupa vigunzi 12,000. Na wastani ni vigunzi 8000 kwa eka. Ukiuza pale pale shambani utapata 800,000/ kwa kila eka.
Ila kama unaweza kulima kwa kumwagilia, utapiga hela vizuri. Nenda Mgama pale karibu na Ihemi ukaone kazi za gobo.
Mkuu Malila, pale galawani mahindi yanastawi vizuri?
Habari mkuu,Pale galawani mahindi hayastawi kwa sababu ni kichanga tupu, ila Mduzi mahindi yanakubali kando ya mto. Niliyaona kwa macho ktk shamba la matikiti maji mwezi novemba 2011.
Pale Galawani ni mifugo zaidi, ila upande wa chini baada ya kuvuka mto kuna ardhi ya kilimo cha mpunga,karanga, tikiti. Huku mwanzoni mwa bonde la Galawani mpunga unaweza kulimwa hasa upande wa kulia wa barabara kama unakwenda shungubweni.
Habari mkuu,
Sasa nilitaka kujua soko la mahindi mabichi kuyauzia shambani,jee naweza miliki hata heka 20 za mahindi na kuyauzia shambani kwa muda muafaka?
Na vp soko la matango pia?jee naweza kuyauzia shambani pia?unaweza kuniambia bei ya wastani ya mazao hayo shambani?
Na vp kilimo cha vitunguu?
Heka 1 naweza pata gunia ngapi???
Mkuu Malila vp soko la mahindi mabichi dodoma? nimelima ekari 70 Banyibanyi (Karibu na mbande) mpango wangu ni kuuza yakiwa mabichi
Sijapita Dom siku kidogo,sijui kama pale mjini watu wanachoma sana kama miji mingine. Ila kwa Dsm mahindi yanachomwa sana,tena sasa hivi wameongeza na utalaam,kama mdomo wako hauna test unawekewa na ndimu na pilipili kabisa. Kama mahindi yanatoka Iringa mpaka Dar, bila shaka hata hayo yako unaweza kupiga bao kwa soko la Dar.
Kwa wale watakaotoa mahindi yao wakati wa low supply wategemee faida kubwa, kuanzia may mpaka july mahindi ni mengi mno.Kuanzia august, september,october na november/desemba, mahindi ya kuchoma dili zuri sana kwa sababu kuna low supply, haya ni yale ya kumwagilia.
Nimependa hii discussion inavyoenda! Ngoja namimi nimtafute partner, sijui nani! Nataka tufunge fruit processing machine pale Chalinze, nahitaji mtu ambaye yuko interested. Tunaprocess hadi parkadging. Karibuni yeyote aliye serious na hili!!
Mkuu Malila nimekupata vema.
Sasa kuhusu mahindi na matango,
Niliweka target sehemu 2,ya kwanza ni IDODI na ya 2 ni KISAKI kule MOROGORO vijijini.
Na matango ni ya kisasa yale ya kuning'inia kwenye kamba ili yasiguse chini.
Sasa mkuu nijulishe nijue kama pale maeneo ya KISAKI ntapata soko la mahindi na matango kuyauzia shambani.
Nimependa hii discussion inavyoenda! Ngoja namimi nimtafute partner, sijui nani! Nataka tufunge fruit processing machine pale Chalinze, nahitaji mtu ambaye yuko interested. Tunaprocess hadi parkadging. Karibuni yeyote aliye serious na hili!!
Ukiweza kupata site pale Chalinze, ni bomba sana. Hata kwa kuanza na miwa/nanasi la kiwangwa sio mbaya. Fikiria na matumizi ya waste za kiwanda chako. Wateja wapo wengi sana. Alongside na juice waweza funga na mashine ya kukamua alizeti.
Mkuu vipi kuhusu Songea Ruvuma kule na kwenyewe vipi lakini maana nina heka zangu kama 150 hivi na sijajua ni pazuri kwa ajili ya alizeti au mahindi??unaweza kunipa mawazo yako au kitu ambacho kitafaaa......
Mkuu Malila vp soko la mahindi mabichi dodoma? nimelima ekari 70 Banyibanyi (Karibu na mbande) mpango wangu ni kuuza yakiwa mabichi
Mkuu Malila nimekukubali! Yaani sehemu zote nzuri kwa kilimo kwanza unazifahamu?! Wewe ni kitu ingine! Lakini mkuu mbona umekomalia sana Alizeti inalipa nini?Ukiweza kupata site pale Chalinze, ni bomba sana. Hata kwa kuanza na miwa/nanasi la kiwangwa sio mbaya. Fikiria na matumizi ya waste za kiwanda chako. Wateja wapo wengi sana. Alongside na juice waweza funga na mashine ya kukamua alizeti.