Masikini_Jeuri
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 6,829
- 1,303
Mkuu Malila nimekukubali! Yaani sehemu zote nzuri kwa kilimo kwanza unazifahamu?! Wewe ni kitu ingine! Lakini mkuu mbona umekomalia sana Alizeti inalipa nini?
Nimepata wazo hapa wakuu!
Tutenngeneze thread imwe kama Dira ama database as ana attachment.......
Humo tuweke
Nini kinastawi wapi? kwa gharama gani ; chanagamoto gani; msimu gani; kwa msaada wa karibu nani atahusika..................tutapiga mbele kwa kila kitu the same thing tuiweke kwenye mifugo na hata madini ama biashara; ni wazo tu limenijia baada ya kukuta aina hii ya maswali ikijirudia lakini kila siku kumekuwa vitu vipya vya kujifunza kwayo..............mtaniambia namana ya kuliboresha wazo hili lakini naamini litatusaidia.
Tukifanikiwa kuwa na data base ya mambo haya tutakuwa tumepiga hatua moja mbele. Naamini wengi tutakubaliana kuwa kuna mapungufu sana ktk utafutaji wa habari muhimu. Kupitia humo tunaweza kuonyesha wapi pilipili mtama inamea, wapi nyuki wadogo wapo, wapi mbuzi wanaozaa watoto watatu wanapatikana, wapi mdung`wa unapatikana, kinyonga wa pembe moja anapatikana wapi.
Habari wana jf.
Nina mpango wa kulima mahindi na matango kwa ajiri ya kuyauza kwenye soko la ndani,
Napenda kujua kama kuna anayejua soko limekaaje?I mean ntafanya biashara au itakula kwangu?nimepata shamba maeneo ya Iringa vijijini na nimepanga kuuzia shambani,jee mahindi mabichi na matango naweza kuuzia shambani kwa bei gani?nimepanga kulima hk 10 za mahindi na 10 za matango!
Naombeni msaada wakuu.
website ya wizara ya kilimo ina ramani inayoonyesha nini kinastawi wapi na wapi kunafaa kupanda nini tunaweza kuanzia hapo kutengeneza data base yetu
Haya tuundeni kamati ya utekelezaji basi aidea ikiwa ya moto
Wewe Malila na kupa cheo cha coordinator kwenye hili!
Songea vyote viwili vinakubali, ila wasiwasi upo ktk soko la mahindi mabichi kama mada ya jamaa ilivyo. Mahindi mabichi hayatakiwi kukaa sana yakishafika sokoni,kumbuka kwa mikoani yakishapoteza test yanatupwa. Mikoani watu wanakula vya leo leo.
Jamani hata ufugaji unalipa sana hasa kama una eneo.mbuzi mkatoliki,kuku wa kisasa,kienyeji wana soko zuri tu.
Asante sana mandieta kwa kuanzisha uzi huu na pia shukrani nyingi zimuendee kila aliyeuchangia uzi huu lakini shukrani za pekee zimuendee Mkuu Malila kwa moyo wa uwazi katika kutoa habari, maarifa na chote anachokifahamu. Nami nimekutumia SMS kukuuliza juu ya Matikiti Maji variety ya PETA NEGRA. Natumaini utanijibu!
Mkuu asante,
Ngoja niingie chaka, nitafute kwa faida yako na ya wengine. 2014 nitaanza kulima tikiti organic.
Mkuu shida yetu waswahili hatujui thamani ya organic tungekuwa tunajua hii kitu ni dili sana nje wenzetu wanathamini sana organic products kuna hadi nguo za organic zinazotengenezwa na pamba iliyolimwa organically
Kisaki ni ngumu kwa usafili kwa mazao yanayohitaji kufika haraka sokoni....kisaki lima Ufuta na alizetiKwa Idodi ukilima matango atanunua nani? Wahehe hawali matango, Hotel zenyewe ziko mbili pale mjini. Idodi lima mahindi,alizeti na mpunga. Matango lima huku kwetu Pwani. Tatizo la Kisaki ni usafirishaji wa haraka wa mahindi yako mpaka kwa mlaji wako ( Morogoro au Dar). Kama si kumwagilia, ni kwamba utakumbana na mafuriko toka Iringa/Dom na Tanga na Moro yenyewe.Kama una uhakika na usafirishaji basi Kisaki sio mbaya.
Kumbuka, jamii yetu ya Kitanzania sio walaji wa Matunda hasa huko vijijini. Je umewahi kuwaona watu hapo Kisaki wanakula Matango kwa kununua? Wanaweza kuwa wanakula sio kwa kuyanunua,bali kwa kuchuma shambani kwao.