MSAADA: Soko zuri la MAHINDI

MSAADA: Soko zuri la MAHINDI

Kwelitupu

Senior Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
111
Reaction score
94
Salaam wakuu,

Nina shamba Morogoro na ni mara ya kwanza nimeanza kulima seriously. Natarajia mwishoni mwa mwezi wa June 2013 nitavuna mahindi. Kwa mahesabu ya haraka haraka natarajia kuvuna approximately 400 bags of maize. Now what is the best (most profitable) way of marketing and disposing the produce i.e. how, where, when?

Naombeni ushauri wenye uzoefu na biashara ya mazao.

Thanx
 
Kwa kuwa upo Moro nadhani Kibaigwa Dodoma itakuwa karibu sana lakini pia kama una usafiri karibu Dar maeneo ya Tandale pia kuna soko zuri
 
Hivi hapo Tandale Gunia moja sh ngapi kipindi kama cha mwezi wa September?
 
Bei nzuri ni mwezi wa february or march mkuu vumilia kidogo hadi miezi ya december na kuendeleya utapata mara mbili ya bei ya sasa ila kama una shida sana unaweza uza nusu ya hao hapo manzese mengine hifazi kama upo dar nenda manzese darajani karibu na benki ya access kuna njia imelekeya kushoto hapo utaona maroli mengi yana mahindi na kuna machine za kusaga sembe ukiwa tayari wewe toa tarifaa humu JF tutakupeleka sokoni but kumbuka kuchangia 5% ya faida kwenye kuboresha JF.
 
Huwezi kupata jibu la swali hili kwa sababu ya Market forces.......Demand & Supply
No fixed price and variation yake ni kubwa sana inaanzia Tzs 66,000 to Tzs 180,000. huwezi ku-project chochote hapo

Heeee!! Mahindi yanafika 180,000???????
 
ila kitu ambacho ungefanya ni kuongeza thamani ya mahindi yako kwa kutengeneza unga halafu uuza,
 
kwa kufanya hivyo unaweza uza bei nzuri
achana na brokers fanya marketing mwenyewe halafu uza
 
Uliuliza bei ya Gunia la Mahindi sokoni Tandale kipindi cha mwezi September.
Soko limeshikiliwa na Madalali na ndo wanaopanga bei,mkulima hana nafasi hapo zaidi ya kusubiri mgao wake toka kwa madalali
 
Uliuliza bei ya Gunia la Mahindi sokoni Tandale kipindi cha mwezi September.
Soko limeshikiliwa na Madalali na ndo wanaopanga bei,mkulima hana nafasi hapo zaidi ya kusubiri mgao wake toka kwa madalali

Nilipoona hiyo range nikasema wastani hapo bei gunia 100,000 haraka haraka nikasema bora niwe mkulima wa mahindi. Ulipokuja kunifafanulia kuhusu bwana dalali bora niwe mchumia kivulini aka dalali hahaha
 
Back
Top Bottom