Msaada: Taa ya kuonesha 'Check Oil' inawaka

Msaada: Taa ya kuonesha 'Check Oil' inawaka

Jaslaws

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
6,016
Reaction score
5,296
Habari najua hapa kuna mafundi wa magari watanisaidia,

Nina gari Harrier hizi 'Second generation' japo yenyewe ni ya muda kidogo. Kuna kipindi nilisafiri kwa muda kidogo hivyo niliipaki kwa muda.

Baada ya kurudi nilimpa kijana akanisaidi kufanya service, baada ya service taa ya oil iliwaka nilipeleka kwa fundi. Fundi akasema shida ni oil pump nili badili oil pump ya kwanza haikupona fundi akasema inawezekana oil pump tuliofunga sio nzima akaibadilisha tena taa ikagoma kuzima.

Kwa namna fundi nilivyomuona niliona kama ujuzi wake umeishia pale na wala shida sio pump. Basi nikachukua gari yangu nikarudisha nyumbani hivi nnavyozungumza gari ipo nyumbani na haijapona..

Kama kuna fundi mzuri hapa naomba anishauri hapa kisha tuwasiliane anisaidie gari inanipasua kichwa hii..

Asanteni.
 
Mkuu we zima hyo taa kama vp, nweis in seriua talk jarbu kwenda kwa fundi mwengne ubaya mafundi wetu weng hawajui.kutengeneza wanajua kubadlisha
 
Habari najua hapa kuna mafundi wa magari watanisaidia.....

Nina gari Harrier hizi 'Second generation' japo yenyewe ni ya muda kidogo. Kuna kipindi nilisafiri kwa muda kidogo hivyo niliipaki kwa muda...

Mwaga oil weka genuine oil na genuine filter
 
Habari najua hapa kuna mafundi wa magari watanisaidia...

Asanteni.
Pole sana mkuu tatizo lako limegawanyika katika sehem kuu mbili..
Mechanical problem na electrical problem..8

Mechanical problem.
Hapo ndio kwanza unazungumzia hiyo pump filter na strainer ukiachana na oil filter ndani chini ya sample kuna chujio tena huwa linaziba.

Fungua mfuniko oil engine. Kisha washa gari harafu angalia oil inaluka luka?? Kama ndio basi oil inapanda shida sio oil pump..

Kama hapana basi oil haipandi je kwa nn haipandi?? Fungua oil filter au switch ya oil..funguo oil filter na angalia kuna oil ya kutosha?? Au fungua switch ya oil na washa gari inatakiwa oil itoke kwa pressure kubwa sana. Kama hakuna oil basi oil pump au strainer chafu imeziba.

Electrical problem hapo inamaana switch mbovu au kama sio mbovu basi imejaa uchafu kiasi kwamba oil ya pressure haiwezi kupenya kwenye oil switch na kupress diaphram ili kuiwezesha switch iweze kufanya kazi yake.

Au switch yenyewe ni mbovu inashort circuit..au oil warning lamp circuit ina short. Kuna sehem waya unagusana na erth /ground nakufanya taa iwake moja kwa moja.. ukitaka kufaham short circuit weka switch on harafu chomoa waya wa kwenye oil switch harafu weka switch on uone kama taa itaendelea kuwaka kama itazima basi cir uit iko powa.
 
Pole sana mkuu tatizo lako limegawanyika katika sehem kuu mbili..
Mechanical problem na electrical problem..8

Mechanical problem.
Hapo ndio kwanza unazungumzia hiyo pump filter na strainer ukiachana na oil filter ndani chini ya sample kuna chujio tena huwa linaziba.

Fungua mfuniko oil engine. Kisha washa gari harafu angalia oil inaluka luka?? Kama ndio basi oil inapanda shida sio oil pump..

Kama hapana basi oil haipandi je kwa nn haipandi?? Fungua oil filter au switch ya oil..funguo oil filter na angalia kuna oil ya kutosha?? Au fungua switch ya oil na washa gari inatakiwa oil itoke kwa pressure kubwa sana. Kama hakuna oil basi oil pump au strainer chafu imeziba..

Electrical problem hapo inamaana switch mbovu au kama sio mbovu basi imejaa uchafu kiasi kwamba oil ya pressure haiwezi kupenya kwenye oil switch na kupress diaphram ili kuiwezesha switch iweze kufanya kazi yake..

Au switch yenyewe ni mbovu inashort circuit..au oil warning lamp circuit ina short.
Kuna sehem waya unagusana na erth /ground nakufanya taa iwake moja kwa moja.. ukitaka kufaham short circuit weka switch on harafu chomoa waya wa kwenye oil switch harafu weka switch on uone kama taa itaendelea kuwaka kama itazima basi cir uit iko powa..
dah nashukuru sana sasa fundi wa kunifanyia haya nampata wapi?
 
tafuta kifaa cha OBDII tatizo la gari utalifahamu mara moja kuliko ufundi wa try and error, utapoteza pesa nyingi mno namna hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli kwa hiyo shida huwezi pima na mashine ikaonyesha na hakuna mashine ya kuweza kuonyesha shida ya hiyo gari zaidi ya kutrouble shoot manually.
 
Kama utakwenda kwa fundi na akasema kakupimia na mashine na katambua shida yako kwa kutumia mashine 800000% kakuibia huyo fundi na sio mwaminifu kabisaa..nategemea akwambie ukweli shida yako lkn sio kwakutokana na mashine..kapima nakutambua shida..
 
dah nashukuru sana sasa fundi wa kunifanyia haya nampata wapi?
Kwani ww upo wapi?? Mkoa gani/wilaya gani.
Kama upo dar naweza kukusaidia kukutambulia tatizo ni nn free of chaji
 
Kwani ww upo wapi?? Mkoa gani/wilaya gani.
Kama upo dar naweza kukusaidia kukutambulia tatizo ni nn free of chaji
dah mkuu nitashukuru sana mie niko dar maeneo ya stakishari ukonga na gari niko nayo hapa!!
 
dah mkuu nitashukuru sana mie niko dar maeneo ya stakishari ukonga na gari niko nayo hapa!!
Okey ungefika ofisini ingekuwa bule lkn huko nje ya ofisi utagaramikia nauli ya kutoka mwenge mpaka huko mkuu kama utaweza hilo nitafika bila tatizo
 
Okey ungefika ofisini ingekuwa bule lkn huko nje ya ofisi utagaramikia nauli ya kutoka mwenge mpaka huko mkuu kama utaweza hilo nitafika bila tatizo
mkuu bila shaka,naku pm
 
Back
Top Bottom