Msaada taa za ABS na Tyre pressure kuwaka muda wote

Msaada taa za ABS na Tyre pressure kuwaka muda wote

Prince Nadheem

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
1,259
Reaction score
1,056
Habari za week end humu jukwaani! Nina gari yangu Toyota Corolla 110 tangu 2011. Sasa tangu j4 na inawasha taa ya ABS na ya Tyre pressure muda wote. Nimeenda kwa fundi, ikazima kwa muda ila kwa sasa imerudi constantly inawaka. Au inawezekana ABS sensors ni chafu au ni kitu gani?? Nimeangalia relay yake kupitia fundi anasema bado ni nzima.

Cc: LEGE, mshana jr
 
Jamani watu mnachungulia tuuuuu mbona sipati msaada ati!!
 
Jaribu kucheck wire wa abs ktk hub ya tire inawezekana umekatika..tatizo kila tire lina wire wake hivyo ni muhimu kutumia mashine ya diagnostic uweze kujua ni hub ya tire la upande upi..
 
Jaribu kucheck wire wa abs ktk hub ya tire inawezekana umekatika..tatizo kila tire lina wire wake hivyo ni muhimu kutumia mashine ya diagnostic uweze kujua ni hub ya tire la upande upi..
Diagnosis machine wanachaji bei gani sehemu ambazo ni very reliable? Maana naona hii ni sensitive case kwa suala la usalama wangu na chombo pia
 
Mkuu kwa kikolorolla 110 usipate tabu nacho kata hivyo viwaya kwenye tyre na abs katembee bleki si zipo?
 
Mkuu kwa kikolorolla 110 usipate tabu nacho kata hivyo viwaya kwenye tyre na abs katembee bleki si zipo?
Mkuu tuheshimiane kwa hilo... Halafu kajifunze spelling na proper writing. Maana post yako sijaelewa zaidi ya dharau tu...
 
Badilisha fundi au garage mkuu ili upate maoni toka kwa fundi mwingine.
 
Njia ya rahisi ya kujua tairi yenye shida ukitaka kusimama ghafla kuna tairi itasota hiyo ndio inashida. Cha kufanya fungua safisha hizo censor kisha peleka kwenye diagnostic machine.

Tyre pressure fuata instruction zilizopo kwenye tyre manufacturer ina specify kiasi cha pressure.
General rule ipo kwenye frame ya mlango itakuonesha tyre size na recommended pressure
 
Pole sana mkuu .kama upo dar naweza kukusaidia kukupimia then spea juu yako. Kama itahitajika .napatikana mwenge kama unaweza fika.

Ila kama upo mbali na dar ni PM namba yako then nitakupa maelekezo ni kipi ukifanye sababu kuandika hapa naweza maliza kitabu kizima na bado usinielewe.

Je huo ugonjwa ulianza kuna kitu chochote ulibadili kwenye miguu kama cv joint ??

vipi ulipo enda kwa fundi alikwambia shida ni nn??
 
Nipo Dar Mkuu!! Nakuja PM kuyajenga. Nitangulize shukurani zangu za dhati kwa msaada wako [emoji120] [emoji120]
 
Mkuu tuheshimiane kwa hilo... Halafu kajifunze spelling na proper writing. Maana post yako sijaelewa zaidi ya dharau tu...
Tatizo moderator humu wanavumilia sana watoto wa darasa la saba. Wanadhani kila saa ni mda wa utani. Mods wakilalamikiwa hawachukui hatua ya maana. Bar ikifanyika adabu na heshima itakuwepo humu
 
Back
Top Bottom