Habari zenu wadau,
naombeni msaada wenu wa kitabibu kuhusu kuzidiwa hasira,
kadri mda wa bunge unavyozidi ndivyo na mimi huzidiwa hasira, nimejitahidi kutolifuatilia na kujaribu kuweka pamba masikioni ila najikuta pamba zimedondoka na luninga inaleta kiyoo chenye picha ya bunge, nazidiwa hasira zaidi nikiona picha ya kiti na wanaoongoza kiti, hasira zinazidi zaidi nikiona picha ya wanaolindwa na kiti hasa wanapovunja kanuni,
jamani nipo serious, naombeni ushauri wenu watalaam maana kadri siku zinavyozidi nahisi kupatwa na mawazo ya kutembea na kisu ambayo ndiyo silaha pekee ninayomudu kuinunua,
asanteni.
mkuu MziziMkavu
nina umri wa miaka 33.
nimeoa.
nina do daily.
dini yangu mwafrika. (sina bahati ya kutekwa na dini za wageni.)
asante kwa ushauri mkuu ila sidhani km ntaweza kuzungumza na hili BANGE lote huko dodoma, nimejaribu pia kwenda pale magogoni mara nyingi ili nionane na meneja wa magogoni niseme yote ya moyoni lakini sikupata bahati hiyo,
Habari zenu wadau,
naombeni msaada wenu wa kitabibu kuhusu kuzidiwa hasira,
kadri mda wa bunge unavyozidi ndivyo na mimi huzidiwa hasira, nimejitahidi kutolifuatilia na kujaribu kuweka pamba masikioni ila najikuta pamba zimedondoka na luninga inaleta kiyoo chenye picha ya bunge, nazidiwa hasira zaidi nikiona picha ya kiti na wanaoongoza kiti, hasira zinazidi zaidi nikiona picha ya wanaolindwa na kiti hasa wanapovunja kanuni,
jamani nipo serious, naombeni ushauri wenu watalaam maana kadri siku zinavyozidi nahisi kupatwa na mawazo ya kutembea na kisu ambayo ndiyo silaha pekee ninayomudu kuinunua,
asanteni.
Mkuu, kama uko Dar, nenda mtaa wa Lumumba opposite na mgahawa wa Falcon pana jengo la rangi ya kijani na manjano limeandikwa "ofc ndogo ya makao makuu......" Ingia humo omba kadi ya uanachama, utalipia hela kidogo then utapewa kadi ya uanachama yenye rangi ya kijani(chani kiwiti), hapo hasira zote zinakwisha!
"IF YOU CAN'T BEAT THEM, JOIN THEM"